Ecobank Tanzania imeendesha semina ya mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’ wenye lengo la kuwasaidia na kuwainua Wanawake Wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa katika masuala mbalimbali ya kifedha na kuwaongezea kipato ili waweze kumudu biashara zao na kuinua vipato vyao.

Mpango huo ni maalum kwa Benki hiyo kuwaelimisha Wanawake hao jinsi ya kufanya biashara hizo sambamba na kuwapa mikopo kwa bei nafuu. Ili kuwa na vigezo ni lazima Wanawake hao Wajasiriamali wawe na Leseni za Biashara na kufungua Akaunti katika Benki hiyo.

Akizungumza  wakati wa kufungua Semina hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa  Ecobank Tanzania, Charles Asiedu amesema mpango huo ni maalum ambao utawafikia wanawake wajasiriamali wengi na  kuongeza mtaji wao, kupata faida na kujinua kiuchumi.

Pia amesema Ecobank imeanzisha mfumo maalum wa kuwaunganisha wafanyabiashara mabalimbali barani Afrika ujulikanao kama "Trade hub" wanatumia Benki hiyoikiwa na lengo la kupanua wigo wa biashara zao ili kuweza kutanuka kimasoko kimataifa  na kuwakutanisha wafanyabiashara mabalimbali ili kuweza kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kupitia huo mfumo.

Amesema kutokana na Takwimu za Benki hiyo zaidi ya asilimia 95 ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa hapa Tanzania ni asilimia 54 zinayomilikuwa na wanawake hivyo mpango huo utaweza kuwainua wanawake wengi ili kuweza kujitegemea kwenye mitani ikiwemo na kukua kiuchumi

"Tangu kuzinduliwa kwa mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’, Ecobank Tanzania imewafikia wanawake zaidi ya 200 ambapo mpaka mwishoni mwa mwaka huu wanatarajia kuwafikia wanawake  wafanyabiashara 500" alisema Asiedu

Ellevate by Ecobank inalenga Biashara zinazomilikiwa na wanawake, Biashara zinazoendeshwa na wanawake, Kampuni zenye asilimia kubwa ya wanawake kwenye ngazi za maamuzi kwenye kampuni hizo,  Kampuni zinazozalisha bidhaa za wanawake kama vile urembo, mavazi nk. 

Mkurugenzi Mtendaji wa  Ecobank Tanzania, Charles Asiedu akizungumza na Wanawake Wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa wakati wa kufungua semina ya mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’ iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu akiwakaribisha wanawake wajasiriamali kwenye semina ya mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’ .
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Ecobank Tanzania, Joyce Ndyetabura akizungumza kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wanawake pamoja na wajasiriamali waliofika kwenye  semina ya mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’ iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Wateja Wadogo na Kati (SME) wa Ecobank Tanzania,  Juma Hamisi akizungumza kuhusu namna ya kufungua akaunti kwenye Benki hiyo wakati wa semina ya mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’  iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi ambaye ni Mkuugenzi wa Kampuni ya TAPBDS, Joseph Migunda akitoa mafunzo ya ujasiriamali na namna wanavyoweza kuimarika katika ukuzaji wa mitaji kwenye mauzo na ununuzi.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali pamoja na wafanyakazi wa  Ecobank Tanzania wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa  Ecobank Tanzania, Charles Asiedu alipokuwa anafungua  semina ya mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Ecobank Tanzania, Charles Asiedu akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ecobank Tanzania pamoja na Wanawake Wajasiriamali mara baada ya kufungua semina ya mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...