KUELEKEA siku ya kifua kikuu duniani jamii imeaswa kujijengea tabia kwenda katika vituo vya afya kupima pindi wanapobaini kuwa na dalili za kifua kikuu ili kupatiwa ushauri wa kitaalamu kwani kufanya hivyo kutasaidia kujitambua na hivyo kuanza kupatiwa matibabu ya haraka ambayo hutolewa bure nchini kote badala ya kuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma katika Hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Dk.Saudan Masawe alipokua akizungumza ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani inayotarajia kufanyika mach. 24 mwaka huu.

DK. Saudan amesema watu wengi wenye dalili za kifua kikuu wamekua wakichelewa kufika katika vituo vya afya ili kupima afya zao kutokana na kuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina hali inayosababisha afya zao kudhoofika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuamini kuwa wamelogwa na hivyo kutumia muda mwingi Kwenda kwa waganga.

Aidha ametoa mwito kwa wananchi kutowanyanyapaa watu wenye kifua kikuu kwani ugonjwa huo unatibika kirahisi endapo mgonjwa atawahi kupatiwa matibabu kwa haraka na kwamba si kila mwenye kifua kikuu ana virusi vya ukimwi (VVU).

Katika kuhakikisha hospitali ya rufaa Mwananyamala imejipanga kukabiliana na ugonjwa kifua kikuu nikatembelea vitengo mbalimbali na kujionea hatua zinazochukuliwa tangu mgonjwa anapoanza matibabu kama inavyoelezwa na wataalamu hao.

Mmoja wa wagonjwa wanapata matibabu ya Kifua Kikuu katika Hospitali hiyo Cornel Malimali wanaeleza mabadiliko makubwa ya afya yake tangu walipoanza matumizi ya dawa.

Siku ya kifua kikuu duniani mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo “KWA PAMOJA TUNAWEZA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU”


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...