Na Mwandishi wetu Dodoma

Wakati Tanzania inaungana na Mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha Siku ya Figo Duniani leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika, amewashauri wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kulinda figo zao.

Dkt. Chandika, ametoa wito huo jijini Dodoma, akisema wananchi wanapaswa wafanye mazoezi kuzingatia mlo usioathiri moyo ili kuzilinda figo.

"Mtindo bora wa maisha unaozingatia milo isiyoathiri moyo utaisaidia kuzilinda figo," amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali.

Siku ya Figo Duniani mwaka huu inaadhimishwa ikiwa na kauli mbiu, 'Afya ya Figo kwa Wote pamoja na Upatikanaji Bora wa Matibabu.'

Dkt Chandika amesema wagonjwa 50 wenye tatizo la figo husafisha damu kwa siku katika Kitengo cha Kusafisha Damu katika Idara ya Magonjwa ya Figo katika BMH.

"Watu wenye tatizo la figo wanasafisha damu mara tatu (3) kwa wiki," ameongeza.

Dkt Chandika amesema mpaka sasa, BMH imeishafanya oparesheni za upandikizaji figo kwa watu 36 toka huduma hii ianze miaka sita (6) iliyopita.

Mwaka 2019, BMH ilikuwa Hospitali ya pili nchini kuanzisha huduma ya upandikizaji figo, lakini ndiyo Hospitali pekee kutoa huduma hiyo bila usaidizi wa Hospitali za nje.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...