NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wamekagua na kuridhishwa na Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala katika Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) ambalo linatarajiwa kumalizika June 30,2024.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi huo leo Machi 18,2024 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deodatus Mwanyika amesema serikali imeongezea uwezo wa kimiundombinu TIRDO ambao walikuwa na majengo chakavu ambayo hayakuwa yanaenda na taasisi hiyo.

Aidha amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iridhihinisha jengo la utawala litengenezwe kwani jengo hilo lilisimama kwa muda mrefu.

Pamoja na hayo Kamati hiyo imeiomba serikali kupitia Wizara kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa kuleta bajeti iliyobakia.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema kwa hatua zilizobaki kukamilisha ujenzi wa jengo hilo, walikuwa na bajeti ya shilingi bilioni 3.4 ambapo mpaka sasa wameshapokea shilingi bilioni 1.54 kwaajili ya ukamilishani wa jengo hilo.

Waziri Kijaji ameishukuru Kamati hiyo kwa kuweza kuisukuma serikali na hatimae kupatikana kwa fedha hizo na ujenzi ukiendelea kutoka asilimia 50 iliyokuwepo mwaka jana na kufikia kwasasa asilimia 73.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika wakitembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika wakimsikiliza Meneja wa Mradi upande wa Mkandarasi (SUMA JKT), Mhandisi Kanali Saul Chiwanga wakati walipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akizungumza jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika walipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika wakitembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika wakitembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Mwenyekiti wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika akizungumza jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika wakimsikiliza Meneja wa Mradi upande wa Mkandarasi (SUMA JKT), Mhandisi Kanali Saul Chiwanga wakati walipotembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika wakitembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Mwenyekiti wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika akizungumza wakati akiongoza Kamati hiyo kutembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza wakati Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kutembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akizungumza wakati Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kutembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.

Wajumbe wa Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakiwa katika kikao na Menejimenti ya Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.
Watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) wakiwa kwenye kikao na Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo mara baada ya Kamti hiyo kutembelea na kukagua ujenzi wa jengo la Utawala la Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) leo Machi 18,2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...