Na Said Mwishehe,Michuzi Blog

KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kimesema Kampuni 60 kutoka China zinatarajiwa kishiriki Kongamano la Kimataifa la masuala ya uwekezaji ambalo linatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam Machi 27 mwaka huu.

Kwa mujibu wa TIC, ni kwamba mbali ya Kampuni hizo za kutoka China,pia wanatarajia Kampuni 120 za nchini Tanzania zimekaribishwa kushiriki katika Kongamano hilo ambalo litakuwa na fursa mbalimbali za uwekezaji na kujenga mahusiano kati ya Kampuni zilizopo nchini na zinazotoka China.

Akizungumza leo Machi 20,2024 jijini Dar es Salaam Ofisa Uwekezaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania anayeshughulikia Dawati la China Diana Mwamanga amesema pamoja na maeneo mengine ya uwekezaji Kampuni zinazotoka China zinalenga kuangalia maeneo ya kuwekeza yakiwemo sekta ya madini,Kipimo, Viwanda ,Afya pamoja na maeneo mengine yanayofaa kwa uwekezaji

Amesema kupitia Kongamano hilo TIC inaamini kampuni hizo zitapata nafasi ya kuelezwa kwa kina fursa za uwekezaji ambazo zipo nchini Tanzania huku Kampuni zilizopo nchini nazo zikipata fursa ya kubadilisha uzoefu katika masuala ya uwekezaji.

Amesema pia kupitia Kongamano hilo wanatarajia pia kuitangaza Tanzania na fursa zilizopo katika uwekezaji huku akifafanua China ndio nchi namba moja nchini katika masuala ya uwekezaji wa viwanda.

"Kwa takwimu ambazo TIC tunazo zinaonesha China ndio inashika namba moja kwa uwekezaji nchini Tanzania.Kumekuwa na uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili na hivyo kuwezesha kuwa na fursa mbalimbali za kiuwekezaji,"amesema Mwamanga.

Ameongeza uwepo wa amani na utulivu pamoja na vivutio vya uwekezaji vilivyopo nchini vimekuwa chachu za nchi nyingi ikiwemo nchi ya China kuwekeza nchini huku akisisitiza TIC imeweka utaratibu mzuri unaohakikisha muwekezaji anapokuja kuwekeza anapata vibali vya kuwekeza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara na Uwekezaji kutoka China, Janson Huang nchini China amefafanua kwamba Kongamano hilo litandelea kujenga uhusiano na USHIRIKI kati ya Kampuni za China na Tanzania huku akisisitiza kupitia Kongamano lililofanyika mwaka jana Kuna Kampuni kadhaa kutoka China zimewekeza Tanzania na nyingine zinaendelea na uzalishaji.

"Mwaka 2023 Kampuni 100 zilishikiri katika Kongamano kama hili ambalo linakwenda kufanyika Machi 27 mwaka huu na kati ya Kampuni hizo moja imewekeza katika hilo viwanda vya dawa."

Wakati akieleza zaidi kuhusu Kongamano la mwaka huu,Huang amesema Jinhua imedumisha uhusiano wa kirafiki wa ushirika na Tanzania katika biashara, uwekezaji na kubadilishana kati ya watu na watu.

Ameongeza kuwa mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania hivyo ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiutendaji na Tanzania, Jinhua imepanga kampuni 60 kutoka China kutembelea Tanzania na kushiriki Kongamano hilo.

"Kongamano la Uwekezaji kati ya China na Tanzania na Kongamano la Kukuza Biashara na Uwekezaji la China (Jinhua) -Tanzania litafanyika jijini Dar es Salaam,limeandaliwa kwa pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania ,Serikali ya Watu wa Manispaa ya Jinhua, Kamati ya CCPIT Jinhua, Chama cha Biashara za China (Tanzania)."

Ameongeza wakati wa kongamano hilo kutakuwa na mazungumzo ya ana kwa ana kati ya kampuni za biashara ya Tanzania na Jinhua yatapangwa na kwamba Kampuni hizo zimejikita katika sekta mbalimbali huku akifafanua kupitia Kongamano hilo kutakuwa na fursa nyingi kwa pande zote mbili.

Awali Meneja Maendeleo ya Wanachama Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA), Kelvin Ogodo ametumia nafasi hiyo liikaribisha Jumuiya ya wafanyabiashara nchini kushiriki katika kongamano hilo kwani China wanakuja kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji.




 

Ofisa Uwekezaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania anayeshughulikia Dawati la China Diana Mwamanga(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Kuhusu Kongamano la Uwekezaji linalotarajia kufanyika nchini Machi 27 mwaka huu ambapo Kampuni 60 kutoka China zinatarajiwa kushiriki.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...