Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipokea picha kutoka kwa Msanii wa Uchoraji kutoka jijini Dar es Salaam, Bw. Abel Mndeba, aliyefika kijana huyo mkazi wa mkoani Mbeya anayefanya shughuli zake Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa amechukua uamuzi wa kuchora picha kwa kutambua mchango mkubwa wa Mhe. Dkt. Nchemba katika kukuza maendeleo ya nchi katika sekta za huduma za jamii na kiuchumi kupitia utafutaji wa rasilimali fedha zunazotumiwa na Sekta za utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea hapa nchini.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika picha na Msanii wa Uchoraji, Bw. Abel Mndeba, aliyefika ofisini kwake kukabidhi zawadi ya picha yake ya kuchora, ambapo kijana huyo mkazi wa mkoani Mbeya anayefanya shughuli zake Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa amechukua uamuzi huo kwa kutambua mchango mkubwa wa Mhe. Dkt. Nchemba katika kukuza maendeleo ya nchi katika sekta za huduma za jamii na kiuchumi kupitia utafutaji wa rasilimali fedha zinazotumiwa na Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kwenye miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisikiliza maelezo ya Msanii wa Uchoraji kutoka jijini Dar es Salaam, Bw. Abel Mndeba, aliyefika ofisini kwake (Treasury Square), jijini Dodoma kukabidhi zawadi ya picha ya Mheshimiwa Waziri inayoelezea utendaji kazi wake mahili katika kusimamia masuala ya uchumi, fedha, ustawi wa jamii na nchi kwa ujumla.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimshukuru Msanii wa Uchoraji kutoka jijini Dar es Salaam, Bw. Abel Mndeba, kwa zawadi ya picha aliyompatia na ka kutambua mchango wake katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii zinazoendelea hapa nchini, baada ya Msanii huyo kumtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...