MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewahakikishia Watanzania kuwa serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kufanya uchaguzi huru na wa haki kuanzia wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2025.

Kinana ameyasema hayo leo Machi 5, 2024, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa salamu akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndg. Samia Suluhu Hassan katika mkutano mkuu wa chama cha ACT -Wazalendo.

"Tunakwenda katika uchaguzi wa serikali za mitaa na baadaye mwakani uchaguzi mkuu. Kumefanyika mabadiliko ya sheria tatu bungeni. Sheria ya vyama vya siasa, sheria ya tume ya uchaguzi na sheria ya uchaguzi.

"Kuna maoni yametolewa na wadau mbalimbali katika kamati za bunge, bungeni...ukiangalia sheria ile baada ya maoni na ushauri kuna mabadiliko makubwa sana.

"Nataka niwahakikishie kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ina dhamira ya dhati katika mwaka huu wa uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka ujao kwenye serikali kuu kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki," amesema Kinana.

Amesema mbali na kupitisha sheria nzuri ya kuhakikisha kunakuwapo uchaguzi huru na wa haki, pia dhamira ya Rais Dkt.Samia kufanikisha hilo inajipambanua katika utekelezaji wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...