




Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mtendaji wa FCS anayemaliza muda wake wa uongozi Francis Kiwanga, amesema Shirika la Asasi za Kiraia nchini (FCS) linajivunia miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuheshimu na kusimamia misingi ya demokrasia.
Kiwanga amesema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya uongozi kati yake na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge aliyechaguliwa hivi karibuni.
Amesema kuwa FCS inajivunia uongozi wa Rais Samia unaoheshimu misingi ya democrasia na uhuru wa watu, ambapo amebainisha kuwa FCS itaendelea kuwa daraja kati ya watu na serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
"Kwetu sisi tunaona ni taasisi inayopigania misingi ya utawala bora, tunahitaji kuendeleza juhudi za kupambania maendeleo ya watu, na hili ni suala la kujikumbusha kila siku" amesema Kiwanga.
Aidha, ameongeza licha ya kuwa anamaliza muda wake amehahidi kuendeleza ushiriano na Shirika hilo na atakuwa balozi kwa kutoa mchango wake pindi atakapohitajika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi à Mkurugenzi Mtendaji mpya, bodi imemwamini kuwa atafanya kazi vizuri na kuendelea aliposhia kiwanga kutokana na sifa alizo nazo na ni kijana" amesema Laay.
Naye Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge, ameahidi kufanya kazi kwa weledi kulingana na taaluma na ujuzi alio nao kwa maslahi mapana ya jamii na serikali kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...