KLABU ya Rotary ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya African Youth Foundation imepanda miche ya miti 1,000 kwenye Msitu wa hifadhi ya Kazimzumbwi iliyopo Mkoa wa Pwani ikiwa ni mojawapo yake ya mkakati wa kuhifadhi mazingira .

Akizungumza na Michuzi Rais wa Klabu hiyo Nikki Aggarwal wakati wa upandaji wa miche amesema kuwa wamepanda miti hiyo kutokana na kuwa na mradi wao wakutoa madawati kwa shule za umma hapa nchini kwani madawati hayo yanatumia mbao hivyo ni muhimu kutunza mazingira pale mti mmoja unapotumika kutengeneza dawati lazima kuwepo na zoezi endelevu la kuhakikisha eneo hilo linaendelea kuotesha miti mingine kwa ajili ya kupata madawati na hewa safi.

Hata hivyo amesema klabu hiyo ina mpango kazi wa kuhakikisha miche 2500 inapandwa katika Jiji la Dar es Salaam sanjari na Walimu 80 kujifunza somo la Tehama ili kueneza elimu hiyo Mashuleni .

Wanachama wa Rotary Klabu Manisha Tanna na Nirmal Sheth wamesema upandaji wa miti hiyo unawapatia wananchi hewa safi pamoja uhifadhi mzuri wa mazingira

Kwa upande wake Afisa Mtendaji kutoka Taasisi ya Africa Asia Youth Foundation amesema wamepanda miti hiyo kwa kushirikiana na vijana 100 misitu hiyo inachangia hewa ya Oxygeni kwa asilimia 80% kwa Mkoa wa Dar es salaam

Ikumbukwe hii ni wiki ya misitu hivyo upandaji wa miti hiyo unaendana sambamba na wiki hiyo na vijana wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha eneo hili linapandwa miti itakayitufaa hapo baadae.
 

Rais wa Klabu ya Rotary Dar Nikki Aggarwal akiendesha zoezi la upandaji miche ya miti 1,000 katika Msitu wa Hifadhi ya Kazimzumbwi Mkoa wa pwani Kulia kwake  Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Africa Asia Youth Joseph Brayton pamoja na Viongozi mbalimbali wa Klabu ya Rotary

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...