Na Angela Msimbira, TARIME

KAMATI Kudumu ya Hesabu za Serikali (LAAC) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule Sekondarii ya Nyasaricho iliyojengwa katika kata ya Binagi, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Mheshimiwa Staslaus Mabula leo Machi 21,2024 uwakati akikagua ujenzi wa shule pamoja na jengo la utawala la halmashauri hiyo.

"Niwapongeze wasimamizi wote waliosimamia ujenzi wa shule hiii, imejengwa kwa viwango vya juu, mazingira mazuri na inaonyesha kabisa ujenzi unaakisi thamani ya fedha iliyotolewa na serikali,” amesema Mheshimiwa Mabula.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa jengo la utawala mheshmiwa Mabula ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Tarime kutomlipa mkandarasi mpaka atakapokamilisha ujenzi wa jengo hilo.

“Kamati haijaridhishwa na ujenzi wa jengo hilo kwa kuwa limejengwa kwa kiwango kinachotakiwa lakini umaliziaji wa jengo hilo hauridhishi.

"Thamani ya jengo la utawala ni shilingi bilioni 2.9, lakini limejengwa kwa gharama kubwa lakini finishing haridhishi kabisa niwatake kuhamikisha hamumlipi mkandarasi hadi hapo atakapokamilisha jenzi".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...