- Atoa agizo la upatikanaji wa huduma ya maji ifikapo Juni, 2024 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ametembelea na kukagua mradi wa maji Same - Mwanga - Korogwe ambao umelenga kusambaza maji katika Miji ya Same na Mwanga pamoja na vijiji 38 kwenye Wilaya ya Same na Mwanga na vijiji vitano katika Wilaya ya Korogwe. 

Wakati akitembelea mradi huo Mhe. Mpango amewaagiza watendaji wa Serikali pamoja na wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili mradi uweze kukamilika kwa muda uliopangwa na wananchi waweze kupata huduma ya maji. 

"Serikali imefanya kazi kubwa kuhakikisha huduma ya maji inamfikia kila Mtanzania, hivyo niwaombe mfanye kazi ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji ifikapo Juni mwaka huu,"  ameeleza Mhe. Makamu wa Rais. 

Aidha Mhe. Mpango ameipongeza Wizara ya Maji kwa kutekeleza mradi huo ambao mpaka umefikia asilimia 87.5 kukamilika kwake.

Kwa upande wake Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amemhakikishia Mhe. Makamu wa Rais kwamba Wizara ya Maji itaendelea na jitihada za kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa muda uliopangwa ili wananchi watakaohudumia na mradi huo wapate huduma ya maji ipasavyo. 

"Nikuhakikishie Mhe. Makamu wa Rais kuwa, Wizara ya Maji imejipanga na hivyo tunasimamia maagizo uliyotupa ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huu unakamilika," ameeleza Mhe. Aweso. 

Mradi wa maji Same Mwanga - Korogwe unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 262 na unatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya 400,000.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi DAWASA, Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema utekelezaji wa mradi huo unakwenda vizuri na kazi inatarajiwa kukamilika ndani ya wakati.

Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Januari 2021 mara baada ya Serikali kupitia Wizara ya Maji kuikabidhi DAWASA kazi ya kutekeleza mradi huu baada ya mkandarasi wa awali kushindwa kutekeleza kulingana na makubaliano.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...