Na Mwandishi wetu, Mbulu

MBUNGE wa viti maalum Mkoani Manyara, Regina Ndege ametoa msaada kwa kukabidhi viti mwendo kwa watoto watatu walemavu wa Wilaya Mbulu.

Watoto hao watatu ambao wanasoma shule ya msingi, awali walikuwa na changamoto ya kwenda shule na kurudi nyumbani kutokana na ukosefu wa viti mwendo vya walemavu.

Mbunge Regina, akizungumza baada ya kukabidhi viti mwendo hivyo amewapongeza watoto hao na kuhakikisha wanavitumia ipasavyo katika matumizi yao.

“Watoto hawa awali walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa viti mwendo ila mara baada ya kubaini hilo tumefanikisha na kuwapatia hivyo kuwasaidia,” amesema Mbunge huyo.

Kwa upande wao, wazazi wa watoto hao walemavu wamemshukuru mbunge huyo kwa kuwapatia viti mwendo hivyo ambavyo vitawasaidia hasa kwenda shuleni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...