Katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani kwa mwaka 2024, wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mjini Mwema wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam ikiwa Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Wekeza kwa Mwanamkekuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa Jamii"

Tarehe 8 Machi ya kila mwaka ni Siku ya wanawake duniani, ambapo siku hii inataka kukumbushia na kutafakari juu ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Irene Mutagaywa amewataka
 wanafunzi walioko mashuleni kujikita katika kutengeneza ndoto zao kwa kusoma kwa bidii hasa masomo ya Sayansi ili kuweza kuendana na teknolojia inayoendelea kukua siku baada ya siku

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Kilikuwa ni chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadaye. Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina la Clara Zetkin. Yeye alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.
Picha mbalimbali  za matukio ya baadhi ya wafanyazi wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo Machi 08, 2024 leo katika viwanja vya Mjini Mwema wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...