TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imewahakikishia Watanzania kuwa inaendelea kukamilisha ujenzi wa miundombinu, hususani katika miradi ya umwagiliaji nchini,ikiwemo mradi wa vijana wa Chinangali na Ndogowe iliyo chini ya Mpango wa Jenga Kesho Iliyobora kwa Vijana ( Building Better Tommorow (BBT); unaosimamiwa na Wizara ya KIlimo.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa, amesema katika mashamba hayo ya BBT, NIRC imehakikisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo mabwawa, visima na mashamba yanakamilika kwa wakati.

Amesema hatua hiyo imekusudia kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha sekta ya kilimo na kupata matokeo chanya katika miradi hiyo ikiwemo` ajira kwa vijana na ukuaji pato la taifa kwa asiliami 10 ifikapo mwaka 2030.

“Miradi ya kilimo kwa vijana BBT Chinangali na Ndogowe kazi inafanyika ambapo kwa upande wa Ndogowe ikiwa ni moja ya miradi ya BBT mkoani Dodoma unaogharimu zaidi ya sh. Bilioni 21.7; Tume ya Taifa ya Umwagiliaji tumehakikisha tunabadili mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia teknolojia ya mabomba badala ya mifereji.

“Tumefanya ukaguzi wa kazi za mkandarasi kwa kuangalia mabomba hayo yanayotoka katika kiwanda na kwenda eneo la mradi ambayo yatawekwa katika kilomita 104 kuanzia bomba kubwa hadi madogo huku mkandarasi akiwa na wajibu wa kutengeneza kilomita 14 za barabarana, kilomita tano za kuingia shambani, ujenzi wa nyumba ya msimamizi wa shamba Pamoja na ujenzi wa madaraja madogo,”alisema.

Bw, Mndolwa amesisitiza kuwa mkataba wa ujenzi huo umeanza mwaka jana na kumekuwa na changamoto ya mvua hali iliyosababisha mkandarasi kusimamisha shughuli za mradi kwa muda, tume imekuwa ikitafuta njia mbadala ya kumsaidia mkandarasi kuweza kufika eneo la ujenzi wa mradi ili uweze kuendelea na kukamilika kwa wakati licha ya changamoto zinazojitokeza ikiwemo kujaa kwa maji shambani hali inayosababisha mitambo na mashine kushindwa kufanya kazi.

Aidha Mkurugenzi Mndolwa alisisitiza kuwa tume inaendelea na ukamilishaji wa mradi wa Chinangali katika mashamba ya BBT kwa ajili ya mashamba ya vijana ambapo ujenzi wa miundombinu ikiwemo mabwawa, visima na usafishaji wa mashamba unaendelea.

“Pia tumeanza ulazaji wa mabomba lengo ni kuingiza maji shambani, katika mradi huo wa Chinangali kazi zinaendelea kwa kasi ikiwemo kufungua shamba ekari 1150 ambapo tayari ekari 210 na nyinginge 56 zimeshalimwa kwa ajili ya maandalizi ya upandaji,”alisema.

Amesisitiza kuwa miradi hiyo yote inakabiliwa na mvua hali inayochangia mitambo kuzama na matumaini ya tume ni kwa sasa wakati ambapo mvua hizo zimesimama kuharakasha utekelezaji wa miradi.

Amesema NIRC itahakikisha miradi hiyo yote inakamilika kwa wakagti na kufikia lengo la Rais Dk.SamiaSuluhu Hassan katika kuchochea ukuaji wa uchumi.

Naye Meneja wa Mradi wa Chinangali kutoka NIRC, Mhandisi Saidi Husein Ibrahim alisema mradi huo uliopo wilaya ya Chamwino takribani km 45 kutoka Dodoma mjini ukihusisha vijana wa BBT shamba limegawanyika katika katika sehemu nne, ikiwemo sehemu ya hekari 300 ambazo zinatumika na wakulima wa zabibu.

Pia kuna hekari 220 na hekari 400 ambapo kati ya hizo hekari 1150 zinatumika na vijana wa BBT chini ya Waizara ya Kilimo.

Amesema jukumu la tume ni kuhakikisha miundo mbinu ya umwagiliaji inakamilika chini ya Mkandarasi Mkuu Nakuroi mwenye jukumu la ujenzi wa uzio wenye umeme katika eneo lenye urefu wa km7.8 kuzunguka hekari 1772, ujenzi wa nyumba 46 na nyumba mbili za wataalamu.

“Pia mkandarasi huyo ana jukumu la kusafisha eneo la shamba hekari 1400 na jukumu la mwisho ni kujenga miundo mbinu katika hekari 220 na katika hatua hiyo ujenzi wa nyumba zimekamilika kwa asilimia 100 na ujenzi wa nyumba ya pampu na mabwawa yamekamilika kwa asilimia 90 huku mabwawa ya awamu ya kwanza yamekamilika mawaili na kila moja lina ujazo wa lita milioni 20. Aidha jukumu la nne la mkandarasi Nakuroi ni kusafisha eneo la shamba lenye ukubwa wa hekari 1150 na jumla ya hekari 220 zimesha safishwa.Usafishaji umegawanyika katika sehemu ambayo ni kuondoa majani na mibuyu 1465 na zaidi ya mibuyu 400 imeshaondolewa,”alisema

Ametaja jukumu la tano la mkandarasi huyo ni kuandaa shamba na kupanda na jukumuhili limefikia zaidi ya asilimia 90 kwani zaidi ya hekari 390 zimepandwa zao la alizeti.

Mmoja wa vijana ambao ni wanufaika wa mradi wa BBT Chinangali, Yona Remero amesema maendeleo ya mradi ni mazuri hususani katika uchimbaji wa mabwawa, uchimbaji wa visima, hadi sasa kuna visima zaidi ya tisa ambavyo vimekamilika.

“Tunategemea baada ya kukamilika kwa mradi huu tutafanikiwa katika umwagiliaji kwani kilimo cha sasa kinahitaji umwagiliaji kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa tunashukuru NIRC kwa kazi kubwa inayofanya ikiwemo ujenzi huo wa miundombinu ya umwagiliaji na uandaaji wa mashamba .Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...