Na. Mwandishi wetu,Jeshi la Polisi-Arusha.

Katika kuhakikisha Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linatoa huduma kidijitali, Benki ya NMB imeunga mkono Jeshi la Polisi Mkoani humo Kwa kutoa kompyuta pamoja viti ambavyo vitatumika katika shughuli mbalimbali za Jeshi hilo.

Akipokea vifaa hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo pamoja nakushukuru Benki hiyo kwa msaada huo, amesema vifaa vilivyotolewa vitakuwa msaada Mkubwa katika kutoa huduma bora na za kisasa kwa Wananchi.

Kamanda Masejo ameongeza kuwa vifaa hivyo vitaongeza ufasini katika utendaji wa kazi wa Jeshi hilo ikizingatiwa kuwa Mkoa huo unaendelea na mradi wake wakufunga kamera za kisasa katika Mitaa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha usalama wa Jiji hilo.

Kwa upande wake Meneja wa benki ya NMB tawi la Clock Tower Arusha Bw. Praygod Mphuru amesema kuwa wametoa vifaa hivyo kuunga juhudi kubwa za Jeshi la Polisi za kuhakikisha Wananchi Mkoani humo wanakuwa salama.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...