*Mchechu aahidi daraja la ushirikiano na taasisi hizo katika kuleta maendeleo


Na Chalila Kibuda,Muchuzi TV

Serikali imesema kuwa Taasisi ambazo umiliki wa serikali chini ya asilimia 50 zinatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi kutokana na mchango wake.

Hayo aliysema Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt.Natu El-Maamry wakati akifungua mkutano wa siku tatu kwa taasisi ambazo serikali ina umiliki wa chini ya asilimia 50 ulioratibiwa na Msajili wa Hazina (TR) uliofanyika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere Kibaha,mkoani Pwani

Dkt.Mwamba amesema kuwa taasisi hizo licha ya umiliki wa serikali chini asilimia 50 ni wajibu wetu kushirikiana kutokana na mchango wao kuwa mkubwa katika mapato ya serikali..

Aidha amesema kuwa katika mkutano huo na taasisi hiyo wataangalia mambo mbalimbali na mwisho wa siku mwanga utaonekana.

Hata hivyo amesema kuwa mkutano huo ndio utatoa picha kwa serikali na Taasisi hizo kuendelea kujijenga na kuendelea kuchangia Serikali.

Nae Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amesema mkutano huo ni muhimu sana katika kupitishana na taasisi hizo kutokana na mchango wao wanaotoa kwa serikali.

Amesema kuwa katika mageuzi wanayotaka kwa sasa katika Taasisi hizo na kuongeza mapato yasio ya kodi ambao utakuwa utaratibu wenye tija.

Mchechu amesema kuwa taasisi hizo hata gawio zinatoa kubwa kuliko hata zile zenye umiliki wa serikali asilimia 100 hali ambayo lazima kukutana na kujadili pamoja.

Aidha mchechu amesema kuwa mkutano huo utakuwa na mwendelezo katika kuendelea kujijenga.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, aliipongeza Ofisi ya Msajili kwa kukutana na Taasisi na Mashirika ambayo Serikali ina hisa chache la kwanza kufanyika tangu kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964 na kwamba huo ni muendelezo wa kudumisha ushirikiano baina ya Serikali na Wawekezaji.

“Namshukuru Msajili wa Hazina kunialika kuja kuhudhuria ufunguzi wa mkutano huu na kunipa fursa ya kujifunza kutoka kwa kila mmoja miongoni mwa Wajumbe wa Bodi na Maofisa Watendaji Wakuu wa taasisi na mashirika shiriki, katika kujadili pamoja njia za kufuata katika kukuza Uchumi wa Taifa.Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Natu El Maamry, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoa wa Pwani.
Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu baina ya Ofisi ya Msajili Hazina na Wakurugenzi wa Bodi na Maofisa Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ambayo Serikali ina hisa chini ya asilimia 50, uliolenga kutambulisha vipaumbele vya Serikali katika kujenga Uchumi imara kwa kuongeza mapato .
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Natu El Maamry, (kulia) akipeana mkono na Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...