Na. Mwandishi wetu, Mwanza

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuendeleza ujenzi wa kitega uchumi ambacho ni Hoteli yenye hadhi ya nyota Tano jijini Mwanza (Mwanza Tourist Hotel) ambao ulisimama kwa takribani miaka nane.

Akizungumza Machi 18, 2024 Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq, amesema ujenzi huo ukikamilika utachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya mkoa wa Mwanza na Taifa kwa ujumla.

Awali, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba Mwaka huu na utazalisha ajira zaidi ya 250.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Hoteli hiyo inajengwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na itakuwa na uwezo wa kuhudumia wageni kutoka Mataifa mbalimbali.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba ameihakikishia kamati hiyo kuendelea kusimamia ujenzi wa Hoteli hiyo ili ukamilike kwa wakati.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...