Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Abubakari Mwassa ametunukiwa Tuzo ya Utendaji Kazi uliotukuka katika kutatua na kushughulikia changamoto kwenye Sekta ya Biashara na Uwekezaji katika Mkoa wa Kagera.

Mhe. Fatma Mwassa amekabidhiwa Tuzo hiyo Ofisini kwake mapema Machi 18, 2024 na Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw. Vincent Minja aliyefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera akiambatana na uongozi wa Chemba wa Mkoa wa Kagera.

Awali Mhe. Fatma akieleza Hali ya Uwekezaji na Biashara ilivyo kwa Sasa Mkoani Kagera, pamoja na mambo mengine alimuhakikishia Bwana Vincent juu ya Mkoa Kagera kuwa na maeneo ya kutosha na yenye Tija kwa Uwekezaji na Biashara ya aina yoyote sambamba na Ukuaji wa Uchumi wa Mtu Mmoja Mmoja na Mkoa kwa Ujumla.

Katika kuendelea kuimarisha Sekta ya Biashara, Mkuu wa Mkoa Hajat Fatma amesema kuwa kwa sasa Miundo mbinu inazidi kuboreshwa huku akitaja Ujenzi wa Barabara za Lami kwa ajili ya Usafirishaji, Ujenzi wa Meli kubwa ya Mizigo, Uboreshaji wa Bandari za Bukoba na Kemondo, pamoja Uboreshaji wa Njia ya anga ikiambatana na Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Omukajunguti, kitakachoanza kujengwa hivi Karibuni.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...