KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji ya Mitaji ya Umma (PIC) imeitaka serikali kuakikisha fedha zinazotakiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi nchini zinatolewa kwa wakati ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa muda uliopangwa na hivyo kuleta tija iliyokusudiwa katika maendeleo ya taifa

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti na Kamati hiyo Mhe. Deus Sangu (Mb) wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi katika eneo la Magomeni Kota awamu ya pili jijini Dar es Salaam.

Aidha Mhe.Sangu amesema serikali imewekeza takribani bilioni 88 katika mradi huo unaosimamiwa na wakala wa majengo Tanzania (TBA) ambao kukamilika kwake utasaidia kupunguza adha ya makazi kwa wananchi na vilevile kuongeza mapato ya serikali.

"Katika kikao chetu na Menejimenti ya TBA tumepata fursa ya kuoneshwa mpango wa ujenzi wa majengo ya makazi katika eneo hili la Magomeni Kota ambapo tumeshuhudia jengo moja limekamilika na jengo la pili likiwa limefikia 96%" amesema Mhe. Sangu.

Vile vile Mhe. Sangu amepongeza uwekezaji huo uliofanywa na TBA kuwa unakwenda kutatua changamoto ya makazi kwa wakaazi mbalimbali wa jiji la Dar es Salaam kwa kupata makazi ya uhakika.

Pia Mhe. Sangu ameitaka Serikali kuhakikisha inatoa fedha kwa wakati ili kukamilisha mpango huo wa ujenzi wa majengo matano katika eneo hilo la Magomeni Kota kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa makazi kama ilivyokusudiwa.

Aidha, Mhe. Sangu ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuruhusu kufanyika uwekezaji ambao unagusa wananchi wa hali zote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TBA Arch. Dkt. Ombeni Swai ameishukuru Kamati kwa kufanya ziara hiyo na kuahidi kuendelea kuisimamia Menejimenti ya TBA katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...