Na Jane Edward, Arusha

Nchi ya Somalia leo tarehe 4/3/2024 imeandika historia Rasmi kuwa mwanachama wa nane wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo imeelezwa kuwa itasaidia suala Zima la msukumo wa changamoto za ajira kwa wananchi wa EAC kwa kuweka usalama hususani katika masuala ya biashara.

Aidha kutokana na kikao cha Wakuu wa nchi kilicho fanyika Jijini Arusha tarehe 25 mwezi Disemba mwaka Jana waliamua kuweka Rasmi Somalia kuwa mwanachama.

Dkt.Peter Mathuki ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akizungumza katika katika sherehe fupi ya kupandisha bendera na kupokea hati za unachama wa EAC Jijini Arusha amesema soko la Jumuiya limeongezeka na kuwa na watu takribani milioni 350 kwa Sasa.

Amesema kiwango cha ukuaji wa pato la EAC limeongezeka kutoka Dolla bilioni 2.5 Hadi Dola bilioni 3 na kuongeza soko la ajira kuondoa changamoto za ukosefu wa ajira kwa nchi wanachama na ongezeko la bidhaa .

Akiongelea suala la usalama Dkt.Mathuki amesema kuwa kuongezeka kwa soka hilo la watu milioni 350 kutaondoa changamoto za upungufu wa ajira na kupelekea wananchi kuchangamkia uzalishaji wa bidhaa kuuza katika soko hilo.

"Hii ni Moja ya kuondoa changamoto za ajira na kurudisha Hali ya usalama katika mataifa ya Jumuiya ikiwa soko la Jumuiya kwa Sasa Lina watu takribani milioni 350 uzalishaji wa bidhaa utaondoa upungufu na kuzalisha ajira hivyo kuwepo kwa usalama katika nchi zetu"

Kwa Upande wake Waziri wa Habari wa Somalia Daud Aweso amesema wanayofuraha Kubwa kukamilisha safari ndefu ya miaka 12 na safari hiyo ilikuwa na Kazi Kubwa ilikuwa na changamoto lakini hawakuchoka kufikia hatua hiyo ya kukamilisha utaratibu wa mwisho wa kujiunga na EAC.

Alisema Jumuiya hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa Somalia na nchi zote wanachama kwa kuwa nchi ya nane kujiunga na Jumuiya hii na tunaleta mchango Mkubwa tutakaotoa kuleta maendeleo ndani ya nchi zetu katika uchumi biashara n.k.

Ameeleza kwamba changamoto zipo ndani ya Somalia wataendelea kuzifanyia kazi na Kwa mwaka uliopita Kuna mambo mengi tulioyafanya kuhakikisha tunawapa Picha nzuri wanachama wengine kukiwa na wanachama zaidi ya 350.

Awali akizungumza Jbril Abdirashid ambaye ni Waziri wa viwanda na biashara wa Somalia amesema wanayofuraha kuwa sehemu ya nchi nane za Jumuiya hiyo ya EAC na wanashukuru kwa kukaribishwa Rasmi na kuahidi kushirikiana na nchi wanachama za Jumuiya hiyo ili kukuza uchumi. 

 Bendera ya Jamuhuri ya Somalia ikipandishwa juu kuashiria Kujiunga Rasmi katika Jumuiya hiyo.
 

Katikati ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr Peter Mathuki akiwa ameshikilia bendera ya Jumuiya hiyo pamoja na uwakilishi wa Jamuhuri ya Somalia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...