Dar es Salaam Jumapili 10 Marchi 2024. T-MARC Tanzania imeungana na taasisi zingine nchini Tanzania kusherekea siku ya wanawake Duniani. Siku ya Kimataifa ya Wanawake uadhimisha kote duniani na hutumika kama kichocheo cha hatua za kimataifa kuelekea usawa wa kijinsia, vile vile utoa fursa kwa serikali, mashirika na watu binafsi kufanyia dhamira yao ya kukuza haki na uwezeshaji kwa wanawake.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati sherehe hizo, Mkurugenzi wa Utawala T-MARC Tanzania Riziki Nahum alisema ‘kwanza kabisa tunapongeza juhudi zinazofanywa na wanawake katika kuijenga familia, jamii, taasisi na nchi kwa ujumla wake, wakiongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan.

Pia Tunafurahishwa sana na ujumuishwaji wa wanawake katika nyanja mbali mbali za kijamii, kisiasa na kiuchumi, ikiwemo nafasi za uongozi katika asasi, taasisi na serikali ambazo zamani zilikuwa zinashikiliwa na wanaume, hii inaonesha ni jinsi gani kama Taifa tunazingatia ujumuishwaji wa wanawake katika maendeleo’.

T-MARC Tanzania kama taasisi ambayo imejikita katika kutoa huduma na bidhaa ambazo moja kwa moja zinagusa Maisha na ustawi wa mwanamke tunatoa wito kwa wanawake wa Tanzania na duniani kote kuzidi kujiendeleza na kujiamini kuwa wanaweza kufanya chochote na kufika popote wanapotaka, na hasa wakiweka juhudi na kuzingatia kanuni za kimaendeleo. #T-MARC Tanzania #USAID #UNWomen #Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

 

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya T-MARC Tanzania Tumaini Kimasa akiongea na wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Idara ya mahusiano na mawasiliano T-MARC Tanzania Lilian Mallya akichangia mada wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

 

Wafanyakazi wa T-MARC Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kusherehekea siku ya wanawake duniani.

 

Baadhi ya wafanyakazi wa T-MARC Tanzania wakifuatilia kwa umakini sherehe za wanawake Duniani zilizofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...