Katika Kuelekea siku ya wanawake Duniani Wakuza Mitaala wanawake kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) wametoa mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa kwa walimu wa baadhi ya shule za Jiji la Dar es Salaam leo Machi 6, 2024 kama sehemu ya kuadhimisha siku hiyo itayofanyika Machi 8, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa TET,Dkt.Aneth Komba amesema kuwa wameamua kurudisha kwa jamii ili waweze kufadika na utaalamu wa watumishi hasa wanawake wanaosherehekea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia.

"Sisi tumeamua kuanza kusherehekea mapema kujitoa kuwapa walimu mafunzo ambayo tuna amini yatawasiaidia katika kazi zao"amesema Dkt.Komba


Mafunzo hayo yamefanyika katika shule za msingi za Oysterbay, Olimpio, Buguruni, Kunduchi, Mivumoni, Kimwani, Chamazi, Majimatitu, Mikwambe, Kigogo, Raha Leo, Kimbiji, King'azi, Tegeta na Anazaki lengo ni kujadiliana mbinu mbalimbali za kufundishia wanafunzi kuhusu Mtaala ulioboreshwa.

Katika majadiliano hayo, walimu kutoka shule hizo walipata nafasi ya kuujua Mtaala ulioboreshwa kwa undani na kutoa mawazo mbalimbali ya namna bora ya kuboresha mbinu za ufundishaji ili Mtaala huo ulete tija kwa mwanafunzi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...