Na Karama Kenyunko Michuzi Tv

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imetoa elimu ya kodi kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Jimbo la Ilala juu ya unuhimu wa kulipa kodi ili kutoa hamasa kwa wafanya biashara na wananchi kulipa kodi na kudai lisiti .

Elimu hiyo imetolewa leo Machi 16, 2024, Ilala jijini Dar es Salaam kwa viongozi wa CCm ngazi zote katika jimbo la Ilala na Afisa Mkuu Msimamizi wa kodi kutoka TRA, Hamad Mterry ambaye amesema kama kodi italipwa kwa wakati basi pato la Taifa litaendelea kukua

amesema kuwa Mamlaka inaendelea kutoa elimu kwa umma ili watu wajue umuhimu wa kudai risiti na kutoa risiti kwa kuwa nchi haiwezi kuendelea bila Mapato kwani hata miradi inayoendelea kujengwa inatokanana na kodi za wananchi na hivyo amewataka viongozi haoo kwenda kutoa elimu kwa wananchi.

"Hakikisha, unaponunua bidhaa dai risiti na unapo uza toa risiti kwani unapopewa risiti tayari sisi kama TRA tumekwisha iona kwenye mfumo wetu unaposhindwa kutoa au kudai risiti unasababisha hasara kwa Taifa." Amesema Mterry

Amesema kuwa wananchi wanapodai lisiti wanaisaidia serikali na Mamlaka ya Mapato kukusanya kodi ipasavyo ili kufikia lengo la kuteleza bajeti ya serikali

Pia Mtery amesema, kwa sasa wanaachana na mambo ya kutumia mashine za EFDA sababu zinaleta usumbufu kwa walipa kodi na hivyo watahamia rasmi kwenye mfumo wa jumbe(sms) kama wanavyofanya DAWASA na TANESCO ili kuondoa changamoto na kuleta urahisi wa kulipa kodi". Ameongeza Mterry

Mterry amesema kuwa Lisiti zenye stika maalamu za TRA zinapotolewa kwenye mashine ya EFD hupeleka taarifa ya mauzo kwenye mfumo wa TRA ambao unawezesha kukusanya kodi.

Kwa upande wake, Mussa Azan Zungu Mbunge wa Jimbo la Ilala pia Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri amesema kuwa elimu hiyo ikitolewa kwa wananchi ni wazi kuwa nchi itapunguza utegemezi wa mataifa ya nje.

Pia amewataka viongozi wa CCM mkoa wa ilala kutumia semina hiyo kama darasa la mabadiliko na kuachana na ukwepaji kodi kwani kunadhoofisha uchumi wa nchi.

"Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu wawekezaji kwani ndio walipa kodi wakubwa,ilikukuza uchumi wa nchi ni lazima ya kaisari yalipwe na ndipo tutapata maendeleo"Zungu

"Tumeamua kufanya semina hii kwa Viongozi wetu hawa kwa kuwa ndio wanaokaa na watu ndio wanaoweza kuzisaidia hizi Mamlaka kuelezea umuhimu wa kulipa kodi" amesema Zungu.

Amesema kuwa viongozi hao wana mawasiliano na mahusiano na wananchi hivyo wakishabeba ajenda ya kudai lisiti hakuna atakayekwepa kulipa kodi.

"Viongozi hawa wanatoka kwenye mitaa yote ya Ilala kama mnavyofahamu Wilaya ya Ilala ndio walipaji kodi wakubwa kwenye taifa letu hivyo leo wanavyofundishwa hapa nao wanarudi kwa wanachi kutoa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi" amesema Zungu.

Amesema umuhimu wa kulipa kodi umelezwa kwenye vitabu vyote vya dini na kwamba Serikali ya Tanzania itajikomboa kutoka kwenye mikono ya utegemezi wa mataifa mengine kimaendeleo.

"Vitabu vyetu vya dini vinaeleza umuhimu wa kulipa kodi ya Mungu iende kwa Mungu ya Kaisari iende kwa Kaisari sasa hii ni ya Kaisali na Kaisari ili atoe huduma kwa wananchi ni lazima akusanye Kodi ili kuondoa utegemezi wa mataifa ya nje lengo kuu la Rais Samia kupunguza utegemezi kutoka nje na wananch wajivunie maendeleo yetu kwa kulipa Kodi"

Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Saidi Side
amesema kuwa CCM imetoa wajibu kwa viongozi kujua umuhimu wa kulipa kodi ili waweze kuhamasisha na kutelez Ilani ya Chama iliyobeba miradi mikubwa na muhimu nchini.

"Wilaya ya Ilala ndio chimbuko la mapato makubwa kwa upande wa kodi kwa hiyo viongozi wa chama kwenye Wilaya yetu wanaowajibu mkubwa wa kupata Elimu hii ili wao wenyewe walipe kodi na wahamasishe wangine walipe kodi kubwa zaidi tumefundishwa na TRA kudai lisiti"


 

Hamad Mterry Ofisa Msimamizi Mkuu wa kodi kutoka TRA, akitoa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa  viongozi wa CCM Jimbo la Ilala. Mafunzo hayo yamefanyila leo Machi 16, 2024 jijini Dar es Salaam
 

Mussa Azan Zungu , Naibu Spika wa Bunge la Tanzania pia Mbunge wa Jimbo la Ilala akiwaelezea viongozi wa CCM jimbo la Ilala umuhimu wa kulipa kodi wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na TRA leo Machi 16,2024 jijini Dar es Salaam

Baadhi ya watumishi kutoka TRA na viongozi wa CCM wakifuatilia mafunzo ya Elimu ya Kodi kutoka kwa Ofisa Msimamizi Mkuu wa Kodi, Hamad Mterry (hayupo pochani) yaliyotolewa leo Machi 16,2024 kwa viongozi wa CCM jimbo la Ilala.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...