Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utafiti,Machapisho na Ushauri Prof.Pendo Kasoga ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha UDOM ndaki ya TEHAMA na Elimu Angavu Dkt.Rukia Mwifunyi ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Ang'avu Dkt.Florence Rashid ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito leo Machi 18,2024 jijini Dodoma.

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Lughano Kusiluka amezindua mpango wa ukusanyaji data za wamama wajawazito ambazo zitasaidia kutengeneza moduli itakayosaidia wajawazito wengine kujua vitu hatarishi wakati wa ujauzito ili kupunguza matatizo yanayotokana na mimba kuharibika na matatizo mengine wakati wa ujauzito.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo Machi 18,2024 katika chuo hicho Prof. Kusiluka amesema mradi huo unalenga katika matumizi ya teknolojia ya akili bandia katika kutatua changamoto mbalimbali zimazoikumba sekta ya afya hasa upande wa wakina mama wakiwa wajawazito.

Amesema wataalamu kutoka UDOM kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na hospitali ya taifa Muhimbili waliandika wazo la mradi huo na kulipeleka kwenye shirika linaloitwa LACUNA la Marekani ili kuomba fedha kwaajili ya kutengeneza mfumo huo.

“Wahudumu wetu katika afya kwamaana ya madaktari, manesi na wakunga waweze kutabiri kabla ya hatari haijafika kuhusu hali ya afya ya mama mjamzito,”amesema.

Sambamba na hayo amaeongeza kuwa lengo la muda mrefu ni kuokoa maisha ya wakina mama pamoja na watoto pamoja na kuipongeza Serikali kwa jitihada zake inazozifanya kuendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kutoa huduma bora kwa watanzania.

Amesema uanzishwaji wa mradi huo ni sehemu utekelezaji wa mpango mkakati wa chuo cha UDOM pamoja na mpango watatu wa maendeleo ya taifa ambao unatambua kuwa TEHAMA ni nyenzo muhimu katika kutatua changamoto ambazo dunia kwa ujumla inazipata.

“Akili bandia ni teknolojia ambayo imekuja huku kwetu lakini haina muda mrefu lakini imekuja kwa namna mbili kuna wengine hasa kwa elimu ya juu kuna woga kwamba tutafundishaje na tutajuaje kama wale tunaowafundisha watatumia atatumia akili bandia kweli ni wao walioelewa hiyo ni aina moja ya changamoto,"amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya utafiti, machapisho na ushauri Prof. Pendo Kasoga ameeleza kuwa 18% ya wanawake wote kati ya miaka 15 - 49 Duniani hasa nchini Tanzania wanapoteza maisha wakati wa kujifungua hususani wale walioko mbali na vituo vya Afya.

“Kwa lugha rahisi unaweza kusema ni kati ya wanawake 578 kati ya wanawake 100,000 wanakufa wakati wa kujifungua, sasa tunaweza kuona kuwa hili ni tatizo kubwa kwa wanawake hususani wale walioko mbali na hospitali,”amesema.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha UDOM ndaki ya TEHAMA na Elimu Angavu Dkt. Rukia Mwifunyi amesema mradi huo utafanyika kwa mwaka mmoja pekee ambapo taarifa zitaenda kukusanywa kwa muda wa miezi Tisa.

Amesema miradi huo umejikita katika kuandaa takwimu ambazo zitatumika kutabiri viatarishi ambavyo vinaweza kujitokeza wakati wa kijifungua baada ya kujifungua na wakati mama akiendelea na kliniki.

“Kwahiyo tutaanza kukusanya taarifa za wakina mama kuanzia pale anaanza kliniki siku ya kwanza taarifa zake zitakusanywa na kila atakapokuwa anaenda kliniki na wakati anajifungua taarifa zitachukuliwa na mwezi mmoja baada ya kujifungua na taarifa hizi zitatumika kwaajili ya kutengeneza model ambayo itatumika katika kufanya maamuzi ya kujua huyu mama anastahili kupata matibabu ya aina gani”,amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...