KIKOSI cha Tabora United kesho kinarejea kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Ally Hassan Mwinyi kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa saa kumi kamili (16:00 ) jioni.

Tabora itakuwa nyumbani hapo kesho ikiwa ni baada ya kutoka kucheza mchezo wake Jijini Mbeya Februali 28 mwaka huu dhidi ya Tanzania Prisons nakupoteza kwa magoli mawili kwa moja lililofungwa na Erick Okutu.

Kocha Msaidizi wa Tabora United Henry Mkanwa amesema kuwa kama benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu Goran Kopnovic wamejipanga vizuri kuhakikisha kwamba Nyuki wa Tabora wanapata matokeo mazuri .

Mkanwa ameeleza kuwa wachezaji wote wapo vizuri na kwamba kila mmoja yupo tayari kutumika ili kuleta ushindi ndani ya klabu huku akielezea umuhimu wa mchezo huo ukilinganisha na nafasi Timu iliyopo kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara.

Aidha ameongeza kuwa Tabora United inawaheshimu Coastal Union kutokana na kwamba imekuwa kwenye Ligi Kuu muda mrefu lakini pia hata kwenye msimamo wamekuwa na nafasi nzuri na kwamba itaingia kwenye mchezo huo kwa kuwaheshimu licha ya kuwa wapo uwanja wa nyumbani.

“ Tunafaham umuhimu wa mchezo wa kesho kama timu, kwenye mazoezi tumetimiza majukumu yetu kama walimu, lakini pia tunafurahi kuona wachezaji wetu wote wana Afya njema na hakuna mwenye changamoto , morali na ari ipo ijuu kwa kila mmoja, tunaimani kuwa siku zote timu bora haifungwi mara mbili.

Tumepoteza na Tanzania Prisons tukiwa ugenini, hivyo kesho tutakuwa kwenye uwanja wetu wa nyumbani kuzisaka alama tatu ambapo tunajua mashabiki wetu wamekuwa na kiu kubwa ya kupata ushindi.

Kwa upande wake Banza Kalumba akizungumza kwa niaba ya wachezaji amesema “wapo tayari kwa sababu kitu muhimu wanachokihitaji kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye michezo yote iliyobakia ikiwemo wa kesho kwakuwa itasaidia kutoka kwenye nafasi iliyopo hivi sasa na kupanda kwenye nafasi nzuri.

Imetolewa leo Machi 02, 2024
Na Christina Mwagala
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Tabora Uited.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...