Walimu wa shule za Sekondari Vetenari, Temeke, Sandali na wanafunzi wa shule ya ya Temeke wamepewa elimu ya mbolea na kuombwa kuwa mabalozi wema kwenye jamii zao juu ya matumizi sahihi ya mbolea.

Elimu hiyo imetolewa na wawakilishi wa watumishi wanawake wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ikiongozwa na Gema Nganyagwa Afisa Udhibiti Ubora ikiwa ni moja ya shughuli zinazotekelezwa kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 8 machi, 2024.

Akizungumza wakati wa tukio hilo Diwani wa Kata ya Sandali Mhe. Christopher Mwansasu ameeleza kuwa, Tfra ni taasisi ambayo inayotambua na kushirikiana na jamii inayoizunguka katika hali zote.

Ameeleza kuwa, wamekuwa wakishirikiana sana katika shughuli mbalimbali za maendeleo na ndio maana wameona ni vyema kufika na kutoa elimu ya mbolea kwa wanafunzi wa shule hiyo iliyopo katika jamii yao.

"TFRA wanatambua kuwa elimu inaanzia chini na ndio maana wamechagua kundi hili ili kupanda mbegu inayowaandaa na kuwaonesha fursa zilizopo kwenye tasnia ya mbolea" amesema Diwani Mwansasu.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Temeke, Ingia Mtenga, ameishukuru TFRA kwa kuichagua shule anayoisimamia na kutoa elimu iliyowaongezea uelimu wa tasnia ya mbolea wanafunzi na waalimu wao.

Amesema, shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 2767 miongoni mwao wanafunzi 501 ni wa kidato cha 5 na 6 huku ikiwa na jumla ya walimu 60 na walimu 28 wakiwa ni wanawake.

Katika kuonesha uelewa walioupata kupitia elimu iliyotolewa wanafunzi waliulizwa maswali ikiwa ni pamoja na kutaka kujua tofauti kati ya mbolea za viwandani na samadi na kuhoji ni mbolea ipi inafaa zaidi.

Aidha, walitaka kujua namna Mamlaka inavyowafikia wakulima wa vijijini kwa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea, kujua namna Serikali ilivyojipanga kutatua changamoto za upatikanaji wa mbolea za ruzuku uliojitokeza msimu wa kilimo 2022/2023 na changamoto ya kutokupatikana kwa baadhi ya mbolea pindi zinapohitajiwa na wakulima kwa kutolea mfano wa mbolea za Amidas.

Pia, wanafunzi hao walipenda kujua namna Mamlaka inavyodhibiti mbolea zinazozalishwa nchini lakini pia zile zinazoingizwa kutoka nje ya nchi na kupewa majibu Mujarabu kwa maswali yote yaliyoulizwa kutoka kwa wanawake hao.
 

Waalimu wa shule za sekondari Sandali na  Vertenali wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na watumishi wanawake kutoka TFRA mara baada ya kupata mwaliko na uongozi wa shule ya Sekondari Temeke (ujirani mwema) kuhusu nia ya Mamlaka kufika ili kutoa elimu ya mbolea kwa wanafunzi wa shule yao ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
 

Diwani wa Kata ya Sandali, Christopher Mwansasu (katikati),  Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondali Temeke Ingia Mtenga(kushoto)  na Afisa Udhibiti Ubora wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Gema Nganyagwa (kulia) wakiwa katika picha mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea katika viwanja vya shule ya sekondari Temeke yakiendelea tarehe 5 Machi, 2024 wanawake wakirithisha ujuzi kwa waalimu na wanafunzi

 

Wanafunzi wa kidato wa shule ya Sekondari Temeke wakiwa tayari kwa mafunzo ya mbolea kutoka kwa watumishi wanawake wa TFRA ikiwa ni katuka kuadhimisha siku ya wanawake duniani tarehe 8 Machi, 2024
 

Diwani wa Kata ya Sandali, Christopher Mwansasu akiwa katika picha na watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na walimu wa Shule ya Sekondari Temeke mara baada ya kuhitimisha ratiba ya kutoa elimu ya mbolea kwa walimu na wanafunzi. Hapo ni mbele ya bustani ya mbogamboga na matunda ya shule.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...