Jumla ya Wakaguzi 2O kutoka Tanzania na nchi nyingine za Afrika wanahudhuria kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).

Akifungua kozi hiyo Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Bw. Aristid Kanje amewakaribisha washiriki hao chuoni hapo na kuwahakikishia kwamba CATC ipo katika kuhakikisha wanakamilisha lengo lao kwa kufanikisha kozi hiyo.

Kanje aliongeza kuwa wakati wa uwepo wao katika chuo cha CATC kutumia muda huo kama fursa ya kubadilishana uzoefu miongoni mwao, kwani wote wana lengo moja la kuhakikisha usafiri wa anga unakuwa salama.

Kozi hiyo ya ICAO inaendeshwa na wataalam waliothibitishwa na ICAO, Bi. Millicent Henga kutoka nchini Kenya na Bi. Kagiso Mooketsi kutoka nchini Afrika Kusini .

Kozi hiyo iliyoanza Machi 18, 2024 itamalizika Machi 22,2024 na inahudhuriwa na jumla ya washiriki 20 idadi yao kwenye mabano kutoka Tanzania (11), Somalia (1), Nambia(1), Zambia(3) na Eswatini(4).

CATC moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.

Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Bw. Aristid Kanje akizungumza wakati wa kufungua kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) kwa wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga inayofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)
Mkufunzi kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), Neema Msumi akitoa maelezo mbalimbali kuhusu chuo hicho pamoja na kujitambulisha kwa washiriki wakati wa ufunguzi wa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) kwa wakaguzi wa Kitaifa wa Usalama wa Usafiri wa Anga.
Mkufunzi kutoka  Afrika Kusini  Kagiso Mooketsi akitoa utambulisho pamoja na kuzungumzia kwa ufupi kuhusu kozi hiyo itakavyendeshwa wakati wa ufunguzi wa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)
Mkufunzi kutoka Kenya Millicent Henga  akijitambulisha pamoja na kutoa maelezo mafupi ya kozi zitakazofundishwa kwenye kozi maalum ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) kwa wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga inayofanyika katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Baadhi ya washiriki wa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa usafiri wa anga wakifuatilia hotuba ya kufunguzi iliyokuwa inatolewa na Mkuu wa Chuo cha CATC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo hayo ya ICAO upande wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) Dar es Salaam Bw. Aristid Kanje.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC)  Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na wataalam waliothibitishwa na ICAO, Bi. Millicent Henga kutoka nchini Kenya na Bi. Kagiso Mooketsi kutoka nchini Afrika Kusini, wakufunzi wa CATC Dar es Salaam pamoja na washiriki wa kozi ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) ya wakaguzi wa kitaifa wa Usalama wa Usafiri wa Anga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...