Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda amesema Chama Cha Wastaafu waliopigana Vita ya pili ya Dunia (TLC) kuanza kufanya mashirikiano na Wakuu wa Wilaya na Mikoa kwenye matawi yao ili kukiimarisha na kutunza historia kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

Mapunda chama hicho kwa waliopigana vita hiyo wanazaidi ya miaka 100 ambao kwa sasa wapo wachache vyema wakatumika kutoa historia hiyo katika kuwarithisha uzalendo vizazi vilivyopo.

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama hicho ambao utachagua viongozi wapya ambapo amesema chama hicho ni muhimu katika kutunza historia na kutangaza ambayo vijana wengi hawaifahamu kuwa kuna wazee walipiganana kuwepo kwa amani iliyopo ambao walitanguliza uzalendo kwa nchi yao.

Ameongeza wazee waliopigana vita hiyo wako 52 waliohai hadi sasa kati ya Wazee 15,000 walioshiriki vita ya pili ya Dunia ni hazina kwa taifa na wenye historia na nchi yao wakatumika kueleza yaliyofanyika na umhimu wake

“Tumeambiwa kuwa kwenye vita ya pili ya Dunia mwaka 1939 hadi 1945 ambayo sisi wote hapa tulikuwa hatujazaliwa walienda vitani ni watu 15,000 waliorudi ni takribani 13,000 na hadi sasa waliohai ni 52 na mdogo zaidi ana miaka 100 hivyo ni muhimu kuwaandikia historia kabla hawajafa” Amesema Mapunda.

Hata hivyo ametoa wito kwa waandishi wa habari kuwatafuta Wazee hao waliopigana Vita ya pili ya Dunia na kutengeneza makala ambazo zitawezesha kuweka historia nzuri hususani ya picha ambayo itawasaidia vijana na kizazi kijacho kujua historia ya nchi yao pamoja na kujua kuna watu walijitoa kupigana kufa na kupona.

Sambamba na hayo amewataka kuhakikisha kuwa wanafanya uchaguzi mzuri wa viongozi ambao utaendelea kukiimarisha chama na kuendeleza urithi kwa kizazi cha wzee hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TLC Hamis Yazidu Kwizombe amesema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo na Wazee hao ni serikali kutoa msukumo mdogo huku wakitambua uwepo wapigania uhuru ni miaka 50 hadi 70 hivyo kuna nafasi kubwa yao kutambulika.

Aidha ameiomba serikali kuwasimamia katika kutunza Wazee hao kwani ndio waliobakia na ni tunu ya taifa ambayo imewakutanisha na inayofanya watu wengi kukimbilia Tanzania kama kisiwa Cha amani waliyoipigania Wazee hao.

Amesema lengo la mkutano huo ni kufanya uchaguzi Mkuu wa viongozi wa Chama hicho ambao unahusisha wanachama wa aina nne ambao ni Wazee waliopigana Vita ya pili ya Dunia, Ndugu wa Wazee hao, Wanachama wa heshima na Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa Nchi.

Naye Katibu Mkuu wa Chama hicho Charles Lubala amesema malengo ya chama ni kuhifadhi historia ya Wazee kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho.

Amesema tayari wamewasiliana na Wizara ya Maliasili ambapo wamepewa eneo Dodoma ambalo watajenga makumbusho itakayotumiwa na watu mbalimbali kwenda kujifunza historia ya nchi yao.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda akizungumza wakati akifungua mkutano na Mkuu na Mkutano wa Uchaguzi wa Chama Cha Wastaafu cha Waliopigana Vita ya Pili ya Dunia (TLC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 

Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu cha Waliopigana Vita ya Pili ya Dunia (TLC) Hamis Yazidu  akitoa maelezo kuhusiana na chama hicho kwenye   mkutano na Mkuu na Mkutano wa Uchaguzi jijini Dar es Salaam.
 

Katibu Mkuu  wa Chama Cha Wastaafu cha Waliopigana Vita ya Pili ya Dunia (TLC) Charles Lubala akizungumza  kuhusiana na utendaji wa  chama hicho kwenye mkutano na Mkuu na Mkutano wa Uchaguzi jijini Dar es Salaam.
 

Baadhi ya wanachama wa TLC katika Mkutano Mkuu jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wanachama wa TLC katika Mkutano Mkuu jijini Dar es Salaam.
 

Picha za pamoja za wanachama wa walipigana vita ya pili ya dunia waliokaa katika viti wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda wengine ni wanachama kurithi kutoka kwa wapigania vita hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...