Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma
Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi wameendelea kukumbushwa juu ya maelekezo ya Serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyoyatoa akiwaelekeza kuhakikisha Usimamizi wa matumizi na matunzo ya vifaa vya Moto kwa kufanya ufuatiliaji wa Mara kwa Mara.
Maelekezo haya ya kuwakumbusha Wakuu hao yametolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Jenista Mhagama katika hafla ya kukabidhi magari na pikipiki kwa Wizara na Taasisi zinazotekeleza Program ya kuendelea kilimo na Uvuvi iliyofanyika Leo hii Jijini Dodoma katika mji wa Serikali Mtumba.
Na kuongeza kuwa wasimamie vema na kuvitunza vifaa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
"Nitumie nafasi hii kuwakumbushia Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi kuhusu maelekezo ya Serikali kupitia Mheshimiwa Waziri Mkuu aliyoyatoa tarehe 7 Agosti, 2023 akiwaelekeza kuhakikisha usimamizi wa matumizi na matunzo ya vifaa vya moto kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwani moja ya changamoto tuliyonayo nchini ni utunzaji (“maintenance”) wa vifaa na miundombinu mbalimbali.
"Nihitimishe kwa kuwasihi kuvitumia vitendea kazi hivi vizuri
na kuvitunza ipasavyo ili vituwezesha kufikia malengo yaliyokusudiwa katika Programu yetu. Nitumie nafasi hii kuwaagiza Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi mnaohusika na utekelezaji wa Programu hii kusimamia ipasavyo matumizi na matunzo ya vifaa hivi kwa kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwani moja ya changamoto tuliyonayo nchini ni utunzaji (yaani “maintenance”) wa vifaa na miundombinu mbalimbali".
Kwa upande wake Naibu Waziri wa kilimo David Silinde ambao ndio moja ya wanufaika wa mradi huo amesema kuwa mradi unalenga kufikia kaya laki mbili za wakulima ambao ni sawa na watu milioni moja wakiwemo wazalishaji wadogo na wakati wapatao 1000.
"Program hii inalenga kufikia kaya laki mbili za wakulima sawa na watu milioni moja na wazalishaji wadogo na wa kati wapatao 1000 ambao ni wafanya biashara,Vyama vya ushirika na watu Binafsi".
Aidha Silinde amesema kuwa Wizara ya kilimo imejikita katika kuongeza ushiriki wa Vijana kufikia asilimia 30 na wanawake asilimia 50 katika kilimo biashara,usalama wa chakula na lishe Nchini.
"Kwa upande wa Wizara ya kilimo program ya AFDP inatekelezwa na Wizara makao makuu ya TARI,ASA,NA TOSCI kwa lengo la kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo kwa kuimairisha tuja na uzalishaji wa mbegu Bora za alizeti,mahindi na mazao Jamii ya mikunde hususani maharage na uongezaji wa thamani, kuongeza ushiriki wa Vijana kufikia asilimia 30 na wanawake asilimia 50 katika kilimo biashara, kuimairisha usalama wa chakula na lishe Nchini pia kuongeza mchango katika Pato la Taifa".
Kwa kuongezea pia ameeleza majukumu ya Wizara ya kilimo ikiwemo upatikanaji wa mbego Bora na kutoa miongozo mbalimbali na kuhamasisha Matumizi ya mbego hizo Bora.
"Kwa upande wa Wizara ya kilimo Ina jukumu la kuweka mifumo ya upatikanaji mbegu Bora za mazao ya mahindi,alizeti na mazao Jamii ya mikunde na kutoa miongozo mbalimbali na kuhamasisha Matumizi ya a mbegu Bora kwa wakulima katika Mikoa 11 na halmashauri 41 zinazotekeleza mradi wa AFDP".
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amesema kuwa Wizara yao imeendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha mapinduzi ambapo lengo kuu ni kuongeza mchango wa Sekta Uvuvi kutoka asilimia 1.8 Hadi kufikia asilimia 10 mwaka 2026.
"Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha mapinduzi ambapo lengo kuu ni kuongeza mchango wa Sekta ya Uvuvi kutoka asilimia 1.8 Hadi kufikia asilimia 10 mwaka 2026. Program hii imekuwa chachu ya kuchangia katika mifumo jumuishi ya kuboresha ukuaji wa Uchumi kwa wavuvi na wakuzaji viumbe maji na wadau wanaohusika katika mnyororo mzima wa thamani wa Sekta ya Uvuvi".
Shaaban Ally Othman ambaye ni Waziri wa Uchumi wa Buluu Zanzibar amewapongeza watu IFAD chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwani kupitia mjumuiko wa Uvuvi na wao ni wanufaika.
"Na mimi Waziri nikwambie ukweli nawapongeza Sana wenzetu wa IFAD chini ya Uratibu wa Ofisi yako kwasababu Wizara yangu kupitia mjumuiko wa Uvuvi na sisi ni wanufaika wa Mradi huu wa IFAD".
"Niendelee tu kusema kwa upande wetu tutarndelea kutoa mashirikiano makubwa kwenye Ofisi yako inayotusimamia katika miradi hii kuhakikisha kwamba Serikali na malengo ya Taasisi zetu yanafikiwa".
Magari yaliyokabidhiwa ni 11, pikipiki za magurudumu mawili 20 na pikipiki za magurudumu matatu 3 katika Ofisi ya Waziri Mkuu, gari moja; Wizara ya Mifugo na uvuvi magari 4, pikipiki za magurudumu mawili 13 na pikipiki za magurudumu matatu 3; Wizara ya Kilimo gari moja; TARI magari 2 na pikipiki za magurudumu mawili 3; na ASA magari 3 na pikipiki za magurudumu mawili 4.
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...