Waumini wa dini ya kiislamu wametakiwa kuwa na utamaduni wa kusameheana Kwa kila jambo ambalo wamekeseana baina yao ili kuweza kupata radhi za Allah (S.W) na kupata makazi mema kesho akhera.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla wakati akiwasalimia waumini wa Masjid ABRAWY uliopo Fuoni Mambo Sasa  mara baada ya kumaliza  Ibada ya Sala ya Ijumaa.

 

Amesema kuwa suala la kusameheana kwa waumini pamoja na wanchi kwa ujumla  ndio jambo pekee ambalo linampelekea mwanadamu kupata radhi kutoka kwa Allah (S.W) hasa katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa ramadhan mwezi ambao unamafundisho mengi ndani yake.

 

Alhajj Hemed amesema Ramadhani ni Chuo chenye Kuwafundisha waumini mambo mbali mbali ambayo Mwenyezi Mungu huyaridhia kutoka kwa waja wake ikiwemo ibada hivyo ni vyema waumini kudumisha ibada za faradhi na sunna ili kupata Maghfira kutoka kwa Mwenyezi mungu.

 

Aidha Alhajj,Hemed amewasisitiza wazazi na walezi kuwawekea mazingira mazuri vijana wao katika kufuata maadili mema sambamba na kuwakurubihisha katika ibada hasa kipindi hichi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuweza kuendeleza ibada hata kwenye miezi mengine.

 

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar  amesema vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo ni lazima  kila mzazi na mlezi  kujitathmini katika malezi kwa vijana wao wanaowalea kwani kufanya hivyo kutasaidia kupata wanazuoni watakaoweza kuisimamia nchi pamoja na dini kwa ujumla. 

 

Sambamba na hayo  Alhajj Hemed amewataka wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla kuzidi kuwaombea dua viongozi wao hasa katika kumi hili la Mghfira ili kuiacha nchi yenye neema kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae.

 

 Mapema akitoa Khutba katika Sala ya Ijumaa, Sheh HASSAN HEMED ABDALLA  amewataka waumini wa Dini ya Kiislam kufanya yale yote aliyoyafanya Mtume muhamad (S.A.W) ikiwemo kufanya  ibada kwa wingi za faradhi na za Sunna,  kusaidiana, na kutoa sadaka ili kupata fadhila za kumi hili la maghfira.

 

Amesema kuwa waislamu ni lazima kufanya matendo mema tena kwa taqwa huku wakitarajia kupata fadhila kutoka wa mwenyezi mungu (S.W) kwa kila jambo hasa kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhan.

 

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

Leo tarehe..22.03.2024


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...