Aondoa zuio la awali la mgao wa mawe

Aelekeza Wachimbaji waruhusiwe na mgawo kuanzia kesho tarehe 26.03.2024

Wachimbaji waishukuru Serikali kwa utatuzi wa mgogoro na wenye Leseni za kuchimba dhahabu

Asisitza wachimbaji wadogo wasiondolewe katika maeneo ya uzalishaji

Na mwandishi wetu-Tarime

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Machi 25, 2024 amefika katika eneo la Malera Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wamiliki wa Leseni na Kampuni ya KIRIBO ambao ulipelekea zuio la mgawo wa mawe mpaka baada ya utatuzi wa mgogoro huo.

Waziri Mavunde ametumia takribani saa 6 kutatua mgogoro husika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, watendaji wa wizara na viongozi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara (MAREMA)

“Ni maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya utatuzi wa migogoro mbalimbali katika sekta hii ya madini ambayo inadhoofisha kukua kwa uzalishaji wa madini," amesema Mavunde

Aidha, amezipongeza pande zote kwa kuridhia makubaliano katika hatua ya awali ya kutatua mgogoro huo.

Ameongeza kwamba kwa kuwa kulikuwa na zuio kwamba mgao wa mawe yaliyozalishwa usimame kwasababu ya mgogoro huu, ameelekeza zuio hilo liondolewe na mgao wa mawe uanze kesho mapema tarehe 26.03.2024.

"Pia, hakikisheni katika utekelezaji wa wa maridhiano haya, wachimbaji wadogo hawaondolewi katika eneo hilo na waachwe waendelee na shughuli zao," amesema Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanda amemshukuru Waziri Mavunde kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro husika na kupongeza hatua za kuruhusu mgao wa mawe kwa kuwa hali ya kipato ya wananchi wa eneo hilo ilikwenda chini na mapato ya serikali kutopatikana kwa wakati.

Zaidi ya watu 2000 wananufaika na mgodi huo ambao umekuwa ni shughuli kubwa ya kiuchumi ya wananchi wa Malera.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...