NA
K-VIS BLOG/KHALFANS AID
Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umekabidhi vifaa tiba kwa Chama Cha Wafanyakazi
wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar es Salaam.
Akipokea
vifaa hivyo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, jijini Dar es
Salaam Machi 4, 2024, Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Bernard
Maro ameishukuru WCF kwa msaada huo ambao utasaidia juhudi za Serikali katika
kuboresha utoaji huduma za afya.
Bw.
Maro ameongeza kuwa wakati wote WCF imekuwa ni miongoni mwa taasisi za umma
ambazo zimekuwa zikitenga sehemu ya ilichonacho kusaidia jamii kupitia sera ya
kurudisha kwa jamii.
“Lakini
pia katika utekelezaji wa Sheria yenu iliyoanzisha Mfuko, WCF imekuwa karibu
sana na wananchi hasa wale wanaopaswa kupata huduma mnazotoa,” amesema Bw. Maro
na kuongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za TUGHE ambayo ina jukumu la kusimamia
watumishi wa Serikali na Sekta ya Afya kutoka taasisi za Umma na Binafsi, WCF
imekuwa ikitekeleza kwa vitendo masuala ya Utawala Bora, Huduma Bora na
Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Wateja wa Mfuko.
Awali,
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, alisema, Mfuko umekuwa na ushirikiano
mzuri na chama cha TUGHE tawi la WCF, “Hili lazima niliseme mapema bila ya
kusubiri ‘forum’ nyingine, TUGHE tawi wamekuwa na mchango mkubwa wa kutuletea
mawazo ya kuboresha na kuimarisha taasisi yetu, wamekuwa ni watu wanaoongeza
busara badala ya kuchochea moto pale panapokuwa na viashiria vinavyohitaji
majadiliano” amefafanua
Aidha
Dkt. Mduma amebainisha kuwa ushirikiano kama huo umekuwepo kwa kuwa wanaamini
kuwa chama hicho ni chombo muhimu cha kuusaidia Mfuko katika ngazi za mkoa na
taifa ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wadau wa Mfuko kuelewa huduma zinazotolewa
pamoja na haki zao.
“Kuhusu
siku hii ya Wanawake Duniani, WCF imeamua kuwaunga mkono TUGHE ili kufikisha
mahitaji muhimu kwa makundi mbalimbali yaliyoainishwa wakati huu wa maadhimisho
ya siku Wanawake Duniani.” Alisema Dkt. Mduma.
Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...