Na Janeth Raphael - Dodoma

Katika Kuelekea kilele Cha siku ya wanawake Duniani March 8,Wizara ya Fedha imejikita kutoa Elimu juu utunzaji wa Fedha kwa wanawake na kujiandaa Kuelekea uzeeni.

Ametoa maelezo hayo Bi Faudhia Nombo akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha katika Banda lao mapema Leo hii kwenye ufunguzi wa maonesho Kuelekea siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayoendelea Jijini Dodoma yenye kauli mbiu inayosema: Wekeza kwa wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi kwa Jamii".

"Sisi tuna Banda ambalo litatoa elimu kwa wanawake kuhusiana n utunzaji wa Fedha na kujiandaa Kuelekea uzeeni".

"Unajua wanawake ni jeshi kubwa wapo wanawake wajasilia Mali, Watumishi wa Umma na hata wamama wa nyumbani Ila lengo ni kuwa wanawake wote waweze kujitegemea kiuchumi".

Aida Bi Faudhia Nombo amesema wapo wanawake wengi wanatamani kuungia katika vikundi vingi vya kukopa fedha na wasijue wanatumiaje fedha hizi lakini watakapokuja katika Banda lao watapata elimu ya Matumizi ya Fedha hizo.

"Kama unavyojua kuna wanawake wengi wanaotamani kuingia katika vikundi mbalimbali vya kukopesha fedha lakini wasijue Matumizi ya Fedha hiyo wanayokopa".

"Kwa hivi tunawakaribisha Sana wanawake katika Banda letu waone namna hata kama mtu atakuwa amejiunga kwenye kikundi au kikoba anavyoweza kuipata fedha au kukopa fedha akaifanyia Kazi na kutengeneza maandalizi ya uzeeni,kama atakuwa mjasiliamali, Mtumishi wa Umma au mama wa nyumbani basi apate fedha itakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni"

Ameongeza kuwa wanajua kila mwanamke anatamani kuwa vizuri katika suala la Uchumi ndo Mana wao wakazingatia katika kutoa mafunzo juu masuala ya Fedha.

"Narudia tena kila mwanamke anatamani kuwa vizuri katika suala la Uchumi,kwahiyo sisi Wizara ya Fedha tumeweka Banda hili ili wanawake wote waweze kupata mafunzo ya namna kutunza fedha na kuweza kufanya maandalizi ya kufika uzeeni".

Mbali ya mafunzo hayo ya utunzaji wa Fedha na kujiandaa Kuelekea uzeeni Wizara pia inatoa mafunzo ya Usimamizi wa Fedha Binafsi,Akiba,Mkopo,Bima ya Amana,Kodi na zinginezo nyingi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...