Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

KATIBU MKUU Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Jokate Mwegelo ametoa ya moyoni baada ya kuteuliwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kumteua kushika nafasi hiyo ambapo ameeleza hakutegemea na ameweka historia.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho CPA Amos Makala, Naibu Katibu Mkuu Bara John Mongela,Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Salum Hapi pamoja na yeye mwenyewe, Jokate amesema Kweli maisha ni safari na msingi wake ni maandalizi ya Vijana kupitia nyanja mbalimbali. 

Akifafanua zaidi katika mapokezi yao yaliyofanyika Ofisi za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam , Jokate amesema CCM inabaki kuwa Mwalimu na ni kama Chuo Bora cha kuandaa Viongozi  wa sasa na badaye.

"Kwa unyenyekevu mkubwa, namshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi na Wajumbe wote wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuniamini na kuendelea kunipa heshima hii.

"Zaidi  Rais wetu kwa kuendelea kuonesha imani kubwa kwetu sisi Vijana wa Kike na Kiume.Nafasi hii imeniweka katika historia ya kuwa Katibu Mkuu wa kwanza Mwanamke kwenye historia ya Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Lakini imenipa wasifu na historia njema ya kuweza kutumikia Jumuiya mbili kama Mtendaji Mkuu yaani UWT na sasa UVCCM, Niwahakikishie vijana wenzangu wote kuwa imani kubwa na heshima aliyonipa Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia,"amesema Jokate 

Aidha ameahidi kuwa atailinda kwa wivu mkubwa sana katika kutimiza majukumu yake kwa kushirikiana na vijana wenzake wote wakati mwingine bila kujali itikadi ya Vyama vyao ikiwa lengo ni kuendeleza falsafa ya 4Rs na kumsaidia Rais Dkt. Samia katika adhma yake nzuri ya kuwaletea maendeleo Watanzania wote.

Pia amemshuku  Mwenyekiti wao wa Vijana Kawaida na Makamu wake Rehema Sombi na Baraza zima la UVCCM Taifa kwa kazi nzuri wanayofanya huku akisisitiza anafurahi kuungana nao katika kusongesha gurudumu hilo la taasisi kubwa.

Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wote ambao wamempa salaam zao za upendo na pongezi huku akiwaomba waendelee  kuchapa kazi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...