Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa katika ziara ya Kikazi Mkoa wa Kilimanjaro amefanya Mkutano Mahususi na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Nurdin Babu, Kamati ya Usalama ya Mkoa pamoja na viongozi wa Kata ya Mnadani na Kijiji cha Shirinjoro kujadili kuhusu hali ya sintofahamu iliyotokea tarehe 03/04/2024 wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa katika ratiba ya ukaguzi wa Chanzo cha Maji cha Chemchem ya Shirinjoro iliyoko Wilayani Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.
Katika kikao hicho, Mhe. Nurdin Babu ameeleza kuwa taharuki hiyo ilisababishwa na uelewa hafifu wa wananchi kuhusu shughuli za uhifadhi wa vyanzo vya maji na kutoshirikishwa vyema na kumhakikishia kuwa zoezi hilo sasa linaendelea kushughulikiwa hatua kwa hatua ili kuhakikisha kuwa chanzo hicho kinatunzwa kwa mujibu wa Sheria na wananchi wanashirikishwa ipasavyo kwa hatua zote.
Aidha, kikao hicho, Waziri Aweso amemuagiza Mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Bwana Segule Segule kuimarisha ushirikishwaji kwa wananchi kuongeza ufanisi katika kuijumuisha jamii na viongozi wa maeneo husika katika shughuli zote za uhifadhi wa vyanzo vya maji ili kuepuka taharuki zinazoweza kujitokeza.
Pia Waziri Aweso amepoka taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ya kwamba atakwenda katika eneo hilo akiongozana na viongozi wa Mkoa, Kamati ya Usalama na Mkurugenzi wa Bonde la Pangani kwenda kukutana na wananchi na kuwa na maridhiano ya pamoja.
Katika hatua nyingine Viongozi wa Kata ya Mnadani wamepongeza hatua ya Waziri wa Maji kufika kwa haraka na kushughilikia swala hili na kuahidi kwamba watakaa vema na Serikali ya Mkoa pamoja na Bonde la Mto Pangani na kumaliza swala hili.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...