Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua kampeni mpya ya akiba inayofahamika kama "Shinda Mechi Zako Kinamna Yako" mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi.

 Ujio wa kampeni hiyo inayoambatana na zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za gari mbili aina ya BMW x1, unalenga kuimarisha ustawi wa kifedha miongoni mwa wateja hao sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali katika kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia utoaji wa huduma rasmi za kifedha na  kukuza uchumi jumuishi.

Akizungumzia kampeni hiyo kwenye hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NBC Bw David Raymond alisema inahusisha wateja wa rika zote wanaohudumiwa na benki kupitia huduma zake mbalimbali.

“Tunaposema shinda mechi zako kupitia kampeni hii tunalenga kuitumia falsafa ya mchezo wa soka ambao Benki ya NBC ndio wadhamini wakuu wa ligi tatu muhimu hapa nchini ikiwemo Ligi ya Soka ya Tanzania Bara yaani NBC Premier League. Tunapoingiza falsafa hiyo kwenye maisha ni wazi tunatambua wateja wetu wana ndoto, malengo na maazimio mbalimbali katika kufanikisha maendeleo yao hususani kiuchumi ikiwemo ujenzi, kukuza biashara zao, kusomesha watoto na mengine mengi.

‘’Hivyo basi tukiwa kama benki tunayowahudumia tunaona wazi kuwa tunao wajibu wa kuwasaidia wateja hawa kufanikisha malengo hayo na hiyo ndio maana ya wao kushinda mechi zao. Kupitia mkakati huu tunahusisha agenda ya msingi kabisa ambayo kwanza ni kutoa elimu na kuwashawishi watumie huduma zetu rasmi za kibenki zinazogusa rika na makundi yote ya kijamii kuanzia watoto hadi wazee’’ alifafanua.

Alitaja huduma zinazohusishwa na kampeni hiyo kuwa ni pamoja na akaunti ya Chanua ambayo ni mahususi kwa watoto, Akaunti ya Malengo, Akaunti ya Johari mahususi kwa wanawake, Akaunti ya Mwalimu, Akaunti ya Mshahara, Akauti ya Wajasiriamali, Akaunti ya Wanafunzi, Akaunti ya Kua Nasi, Akaunti ya Vikundi, Akaunti Binafsi na Akaunti ya Biashara.

Akizungumzia zawadi mbalimbali zinazotolewa kupitia kampeni hiyo, Meneja Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC, Bi Dorothea Mabonye alisema kampeni hiyo ya mwaka mmoja inahusisha zawadi za kila mwezi na mwisho wa mwaka ikiwemo zawadi kuu ya gari aina BMW X1 zitakazotolewa kwa washindi wawili, fedha taslimu, zawadi ya safari ya mapumziko nchini Singapore, simu za mikononi, ‘laptops’, friji, tablets za watoto pamoja na majiko ya kisasa ya kupikia.

“Tunawahimiza tu wateja wetu wapya na waliopo wajitokeze kwa wingi wafungue akaunti na waweke akiba zaidi ili waweze kuingia kwenye droo zitakazowawezesha kushinda zawadi hizi,’’ alibainisha.

Nae mmoja wa mabalozi wa kampeni hiyo, Nasry Ramadhani maarufu kama Ujugu ambae ni mjasiriamali aliwekeza kwenye biashara ya kuonesha burudani ya mpira kupitia TV kwenye mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam aliwasihi wajasiriamali mbalimbali wakiwemo vijana kutumia vema fursa hiyo iliyotolewa na benki ya NBC kupitia kampeni hiyo ili waweze kunufaika kupitia faida mbalimbali zitokanazo na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NBC Bw David Raymond (wa pili kushoto) akiwaonesha wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo waandishi wa habari gari aina BMW x1 itakayotolewa kwa mshindi wa kampeni ya akiba "Shinda Mechi Zako Kinamna Yako" ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari.

Meneja Masoko wa NBC Alina Kimaryo (wa tano kushoto) sambamba na Meneja Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC, Bi Dorothea Mabonye  (wan ne kushoto) wakiwaonesha wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo waandishi wa habari gari aina BMW x1 itakayotolewa kwa mshindi wa kampeni ya akiba "Shinda Mechi Zako Kinamna Yako" ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa NBC Bw David Raymond (Kulia) na Meneja Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC, Bi Dorothea Mabonye  (kushoto) wakitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kampeni ya akiba "Shinda Mechi Zako Kinamna Yako" ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari.

Meneja Masoko wa NBC Alina Kimaryo (kushoto) na Meneja Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC, Bi Dorothea Mabonye  (wa pili kulia) wakitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kampeni ya akiba "Shinda Mechi Zako Kinamna Yako" ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakifuatilia hafla ya uzinduzi kampeni ya akiba "Shinda Mechi Zako Kinamna Yako" ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari.

Akizungumzia kampeni hiyo mmoja wa mabalozi wa benki ya NBC, Nasry Ramadhani ‘Ujugu’ (Katikati) ambae ni mjasiriamali aliwekeza kwenye biashara ya kuonesha burudani ya mpira kupitia TV kwenye mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam aliwasihi wajasiriamali mbalimbali wakiwemo vijana kutumia vema fursa hiyo iliyotolewa na benki ya NBC kupitia kampeni hiyo ili waweze kunufaika kupitia faida mbalimbali zitokanazo na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.





Wafanyakazi wa benki ya NBC, mabalozi wa benki hiyo pamoja na waandishi wa habari wakijipongeza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya akiba "Shinda Mechi Zako Kinamna Yako" ya benki hiyo mahususi kwa wateja wake wa aina mbalimbali wakiwemo wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo na wanafunzi. Hafla ya uzinduzi kampeni hiyo imefanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa benki hiyo, wateja na waandishi wa Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...