Na Mwandishi Wetu,Dodoma

WAENDESHA bodaboda jijini Dodoma wametakiwa kuithamini kazi yao na kujijali wenyewe ili kuondoa dhana iliyojengeka kuwa kundi hilo limekuwa likivunja sheria za usalama barabarani.

Hayo yameelezwa na Polisi Kata wa Kata wa Kata ya Uhuru jijini Dodoma, alipokuwa akitoa mada katika semina ya mafunzo kwa bodaboda iliyoandaliwa na Shirika la Amend Tanzania kwa kushika na Ubalozi wa Uswisi nchini.

Mafunzo hayo ya naendelea jijini Dodoma ikiwa na awamu ya pili kutolewa katika Jiji hilo.

Amesema kumekuwapo na dhana kuwa, waendesha bodaboda wengi hawazingatii sheria za usalama barabarani, hivyo kuhatarisha maisha yao, abiria wanaowabeba na usalama wa vyombo vyao.

Kwa mujibu wa polisi Kata huyo, mafunzo wanayo yatoa ni muhimu kwa kuwa yanawawezesha bodaboda kufahamu usalama wao na jinsi ya kuvimudu vyombo wanavyoviendesha wawapo barabarani.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata ya Uhuru Fatma Amri anasema mafunzo hayo kwa kiasi kikubwa yanawasaidia vijana katika Kata yake kujitambua na kuzingatia sheria wanapoendesha vyombo vya moto.

Amewasisitiza bodaboda waliopata mafunzo hayo kuhakikisha waafanyia kazi elimu waliyopewa kwa kuzingatia na kuzitekeleza kikamilifu sheria za usalama barabarani.

Kupitia mafunzo hayo waendesha bodaboda hao walielimishwa kuhusu huduma ya kwanza na umuhimu wake, pia usalama wao katika maeneo yao ya kazi.

Mfunzo hayo ambayo yanatolewa kwa ufasdhili wa Ubalozi wa Uswisi yamefanyika kwa bodaboda kuingia darasani na kwa njia ya vitendo kwa lengo la kuwajengea uwezo maofisa usafishaji wote watakaohudhuria mafunzo hayo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...