Kampuni inayoongoza kwa mahitaji ya usafiri kwa makampuni kwa njia ya mtandao barani Afrika Bolt Bolt Business, imetangaza huduma yake mpya ya Bolt Business Kuponi ili kuruhusu wafanyabiashara/mashirika kushiriki au kulipia kikamilifu gharama ya safari ya mara moja kwa wafanyakazi na wateja wao. 

Kuponi ni sehemu ya Bidhaa ya Bolt Business inayolenga kusaidia wateja walio na mahitaji ya usafiri wa kikazi kama vile usafiri kwa shughuli maalum, kutumika kama motisha kwa wafanyakazi au kusaidia katika kutumika kama motisha kwa wateja watumiapo Huduma za makampuni.

Makampuni ambayo ni wateja wa Bolt Business wataweza kutengeneza kupone moja kwa moja bila msaada wowote na kuzisambaza kupitia barua pepe kwa mteja, mfanyakazi au mshirika ambaye wanatraka aweze kutumia kuponi. Mnufaika anaweza kunakili na kubandika kwenye App yake ya Bolt. 

Wateja wanaweza kuchagua kutoka kwenye aina tatu za kuponi, Kuna Kuponi Bila Kikomo, mtu anayepokea kuponi anaweza kuchukua idadi yoyote ya usafiri ndani ya kikomo cha matumizi kilichowekwa.


Kuponi ya kutoa asilimia iliyowekwa ya punguzo la safari hadi kiasi fulani, kwa mfano punguzo la 25% kwa safari ambayo ugharimu zaidi ya TZS 10,000 na hatimaye kuponi ya kiasi kilichowekwa kulipa kiasi fulani, kama vile punguzo la TZS 5,000 kwenye safari.

Kuponi zinaweza kutumika kwa njia yoyote ya safari za kikazi za Bolt Business na safari za kawaida. Ili kusaidia mahitaji ya usafiri, wateja wa Bolt Business wanaweza kudhibiti kiwango cha punguzo na wakati wasafiri wanaweza kuktumia kuponi. Makampuni ambayo ni wateja wa Bolt Business wanaweza kuona ni kuponi ngapi zimetumika kuptitia ripoti maalum ipatikanayo kupitia Bolt Business Dashboard!

Milu Kipimo, Meneja mkazi wa Bolt Business nchini Tanzania & Tunisia, alisema, “Katika kukabiliana na mahitaji yaliyotolewa na wateja wetu wa Bolt Business nchini tunaelewa hitaji la mbinu iliyoboreshwa zaidi ya kulipia au kugawanya gharama za safari za mara moja miongoni mwa wafanyakazi, wateja watarajiwa na washirika wao wote bila kutumia Bolt Business Team Account ambayo ni maalum kwa wafanyakazi pekee.

 Ndio maana tunaitambulisha Bolt business coupons, bidhaa maalum kwa makampuni ambayo ni wateja wetu ili kuwawezesha kuweza kuitumia kama nyenzo katika ufanisi zaidi wa kutoa motisha kwa wateja, washirika na wafanyakazi wao wote huku wakiweza kudhibiti gharama sambamba na kukuza biashara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...