Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) kimejipanga kuwa katika daraja la juu linalotambuliwa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) katika upande wa vyuo vya mafunzo yaani ‘Train Air Plus Training Centre of Excellence-Platinum’ ifikapo mwezi Disemba mwaka 2024.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari leo Aprili 5, 2024 wakati akizindua Bodi ya ushauri ya CATC jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu Johari ameongeza kuwa chuo cha CATC kilichoanzishwa mnamo Juni 10, mwaka 1985 chini ya sheria ya Usafiri wa Anga namba 13 ya mwaka 1977 tayari kimeshapitia madaraja ya ICAO Train Plus Associate Member mnamo mwaka 2012-2019, ICAO Train Plus Full Member mnamo mwaka 2019, ICAO Train Plus Full Member - Gold mnamo mwaka 2022 baada ya kubadilisha madaraja ya awali ya utambulisho (Associate Member, Full Member, Regional Training Centre of Excellence, Corporate Member) na sasa kuwa Train Air Plus Associate-Bronze, Train Air Plus Associate-Silver na Train Air Plus Full Member – Gold.

Mkurugenzi Mkuu Johari ameongeza pia mbali ya sifa hizo chuo cha CATC pia ni Kituo cha Kimataifa cha Ulinzi wa Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) tangu Julai 2022 ambapo ni chuo cha 9 kwa Afrika na cha 35 Duniani.

Na kuongeza kuwa mbali na sifa hizo za kimataifa pia chuo cha CATC kilipata Usajili wa awali wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (NACTVET) mnamo mwaka 2008 na usajili kamili mwaka 2018, pia kina Muongozo wa uendeshaji wa CATC (The Civil Aviation (Training Centre) Management and Operational rules ya mwaka 2021.

Kuhusu malengo ya chuo Mkurugenzi Mkuu Johari alisema malengo ya TCAA ni kukiboresha chuo cha CATC kutokana na kuongezeka kwa idadi yawashiriki wa mafunzo ikiwemo kujenga majengo ya kisasa, kununua vifaa vya kisasa vya kufundishia na kuwajengea uwezo wakufunzi wake.

“Tayari Serikali imetoa eneo lenye ukubwa wa takribani ekari 18 mnamo mwezi Mei 2022. Serikali kupitia wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2023-24 ilitenga kiasi cha shilingi Bilioni tano kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa chuo cha CATC baada ya upembuzi yakinifu uliokamilika mwaka 2022.” Alisema Johari

Mkurugenzi Mkuu Johari amesema gharama za mradi ni takribani shilingi Bilioni 78 ambapo Serikali imeamua kugharamia mradi wote kwa kipindi cha miaka mitatu. Na kwa sasa mradi upo kwenye hatua za kumpata mshauri mwelekezi kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa chuo.

Wajumbe wa Bodi hiyo ya Ushauri ni Bwana Juma Fimbo – Mwenyekiti, John Njawa – Mjumbe, Bi.Thea Thomas Mtau – Mjumbe, Dkt. Kijakazi Omar Makame – Mjumbe Bi. Harriet Nyalusi – Mjumbe na Bw. Jude Mkai – Mjumbe.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Bw. Juma Fimbo alisema yeye , bodi yake pamoja na menejimenti ya CATC wana deni kubwa kwa watanzania la kuhakikisha kweli chuo hicho kinakuwa katika daraja la Train Air Plus Training Centre of Excellence-Platinum hivyo hawatawaangusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akizungumza na mwenyekiti pamoja na wajumbe Bodi ya ushauri ya Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika makao makuu ya Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akitoa maelezo kwa wajumbe wa Bodi ya CATC kuhusu historia pamoja na maendeleo ya Chuo hicho wakati wa uzinduzi wa Bodi Bodi ya ushauri ya Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC).
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Chuo cha CATC Mhandisi Stephen Mwakasasa akitoa maelezo kwa wajumbe wa Bodi ya CATC kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa kwenye ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) unaotarajia kuanza hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa Bodi Bodi ya ushauri ya CATC.
Meneja Mradi Msaidizi wa Ujenzi wa Chuo cha CATC Mhandisi Swalehe Nyenye akitoa ufafanuzi kuhusu muundo wa Majengo ya Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) kwa wajumbe wa Bodi ya CATC.

Baadhi ya wajumbe wakichangia mada mara baada ya kupata maelezo kuhusu Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Juma Fimbo (kulia) akitoa neno la shukrani mara baada ya kupata ufafanuzi kwa baadhi ya kazi pamoja na miradi mbalimbali ya Chuo hicho
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akiwakadhi baadhi zawadi wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika makao makuu ya Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya ushauri ya Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika makao makuu ya Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Bodi ya CATC kuhusu moja ya madarasa wanayotumiwa na Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) walipotembelea Chuo hicho.
Mkufunzi mkuu wa Kitengo cha Kuendeleza Mitahala (CATC) Neema Senyagwa akitoa maelezo wa wajumbe wa Bodi ya CATC kuhusu mtambo wa kuongozea ndege unaotumika kuwafundishia wanafunzi katikati Chuo hicho walipotembelea Chuo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...