Na Mwandishi Wetu

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kinakusudia kuanzisha mafunzo ya uanagenzi kwa wanafunzi wanaosoma shahada ya masuala ya benki, fedha, metrolojia na viwango, ambayo yatawawezesha kusoma huku wakifanyakazi.

Akizungumza katika siku ya CBE taaluma na programu atamizi jijini Dar es Salaam Mkuu wa chuo hicho, Profesa Edda Lwoga, amesema lengo ni kuwawezesha wanafunzi kuhitimu masomo wakiwa na ujuzi unaohitajika kwenye soko la ushindani wa ajira.

Amesema katika utaratibu huo, mwanafunzi atasoma muhula mmoja chuoni na muhula mwingine kwa mwajiri, ambako atakuwa anapata mafunzo kwa vitendo.

“Kwa hiyo mwanafunzi atasoma mwaka mmoja na nusu chuoni na mwaka mmoja na nusu kwa mwajiri. Tumeshaingia makubaliano na baadhi ya taasisi ambazo ziko tayari kuwapokea wanafunzi kwa mafunzo ya vitendo,” amesema.

Kuhusu uatamizi, Profesa Lwoga amsema lengo la programu hiyo ni kuwawezesha wanafunzi kuwa wabunifu na kutumia elimu ya darasani kutengeneza biashara halisi.

Amesema watakuwa wanapatiwa mafunzo sahihi kuhusu mawazo yao ya biashara, mitaji na kuwaunganisha na wafanyabiashara pamoja na taasisi zinazohusika na ubunifu wao.

"Tayari wanafunzi 282 wameshaanza program atamizi na wameanza kutengeneza bidhaa na mifumo ya kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii".

Naye, Edward Talawa, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Finca, Edward Talawa, ambaye alikuwa mgeni rasmi, katika tukio hilo, amesema moja ya nyenzo muhimu ambayo wabunifu wanapaswa kuwa nayo ni nidhamu ya fedha na kwamba benki yake itatoa nafasi ya uanagenzi kwa wanafunzi wa CBE.

Amesema ubunifu uliofanywa na CBE utasadia kutatua changamoto ya ajira nchini, kwa kuwa itazalisha wajasiriamali ambao watajiajiri na kuajiri wengine.

Mapema, Mkurugenzi Mkuu wa Ushirika wa wajasiriamali wahitimu wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), Revocatus Kimario, alisema wanafunzi wana nafasi ya kupata masomo ya vitendo katika nchi za Ulaya na kuwataka walio katika programu ya uatamizi kuzichangamkia.

Kwenye siku hiyo ya taaluma na program atamizi, wanafunzi wa chuo hicho walionyesha uwezo mkubwa kwenye ubunifu wa teknolojia mbalimbali.

Wanafunzi hao walionyesha ubunifu kwenye utengenezaji wa bidhaa mbalimbali na mifumo mbalimbali ya kiteknolojia inayoweza kutumika kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii.
 

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Tandi Lwoga (kulia) akimkabidhi tuzo mgeni Rasm, Edward Talawa ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa FINCA Microfinance Bank kwa kushiriki siku ya Atamizi (Incubation) na kufungua milango kwa CBE kushirikiana na FINCA Microfinance Bank.

 

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Tandi Lwoga (kulia) akimwelezea mkurugenzi wa Benki ya Finca, Edward Talawa namna wanafunzi walivyojifunza kutengeneza nyenzo zitakazowasaidia katika kutatua tatizo la ajira nchini  wakati wa siku ya taaluma na program atamizi iliyofanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 

Mmoja wa wanafunzi wa CBE walioko kwenye program atamizi akielezea kuhusu biashara yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...