Katibu wa NEC - Oganaizesheni Issa Gavu awaomba wananchi wa Wilaya ya Nkasi kubakiza imani yao ya kiitikadi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuamini kwamba CCM ndio pekee iliyojipanga na kujidhatiti kwa madhumuni ya kuharakisha maendeleo kwa watanzania wote.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara viwanja vya Namanyere Mkoani Rukwa.

Amesema mategemeo ya CCM tunaamini nyie ni waungwana na mtakuwa mmepata nafasi ya kujifunza hivyo wanaamini hawatafanya tena makosa ya mwaka 2020.

Aidha amesema CCM wanawahakikishia kuwa imani yenu haitadondoka na mtaiona kwa vitendo, hisani inalipwa kwa hisani hakuna hisani inayolipwa kwa mabaya."

"Tunatekeleza ilani yetu kwa kupeleka salamu na kutuma ujumbe kwao wapinzani kwamba CCM itakwenda kuchukua nafasi zote walizopoteza."

"Nkasi fanyeni uchaguzi sahihi kwa wakati huu sahii, msirudie makosa mliyoyafanya mwaka 2020. Tunatuma salamu kwa mwakilishi wao wa CHADEMA kwamba muda wake umekwisha na salamu hizo zitatimizwa kwa kuanzia kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka huu 2024". Amesema










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...