NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

CHUO Kikuu Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam ( DUCE ) kimefanikiwa kutoa huduma mbalimbali za ushauri elekezi ambazo zimekuwa na maslahi mapana kwa Taifa na pia zimekuwa zikiongeza mapato ya Chuo yatokanayo na ada inayotozwa kwenye huduma hizo.

Ameyasema hayo leo Aprili 17, 2024 Rasi wa Chuo cha DUCE, Prof. Stephen Maluka wakati akifungua Wiki ya Utafiti na Ubunifu na kuwatembela na kukagua utafiti ambao umefanywa na watafiti katika Chuo hicho.

Amesema huduma za ushauri elekezi zimekuwa zinajenga uhusiano kati ya Chuo, Wizara na taasisi nyingine ikiwemo Mradi wa Kutathmini Ukatili wa Watoto wa Kiume nchini Tanzania yaani Rapid Assessment of Violence Against Boys in Tanzania ambao umekuwa muhimili mkubwa kati ya Chuo na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu.

Aidha ametoa rai kwa watafiti na wavumbuzi kuchunguza changamoto mbalimbali katika maisha ya jamii na kubaini njia sahihi ya kuzitatua.

"Naamini ripoti na taarifa mbalimbali za kila mwaka zinazotolewa kutokana na tafiti zinazofanyika ni msingi mkuu wa majadiliano haya. Ripoti na taarifa ziwasaidie kujadili, kupanga, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo". Amesema

Pamoja na hayo amewataka watafiti na wabunifu kutumia majadiliano hayo kujenga hoja za msingi kwani maoni yatolewayo na wanataaluma kwenye majadiliano hayo husaidia katika kuboresha namna ya kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...