Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro imewataka Wananchi wa Mkoa huo kuwa watulivi wakati Serikali ikiendelea kuchukuwa hatua za dharura kurejesha miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoharibika katika kipindi hiki cha mvua kubwa .

Akizungumzia athari za mvua hizo tarehe 28 Aprili 2024; Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe L. Kyamba ameeleza kuwa tayari Wakandarasi wapo katika maeneo yote yaliyo athirika na kazi ya urejeshwaji wa miundombinu hiyo inaendelea.

"Mvua hizi sio Ulanga peke yake ni Nchi nzima, lakini kwa Ulanga Mwezi Februari liliondoka daraja katika Kijiji cha Mwaya daraja lile liliondoka kwa sababu ya mafuriko tukapeleka daraja la chuma la dharura, tumejenga daraja kwa wiki mbili kwa sasa hakuna shida panapitika"

Ameainisha maeneo mengine yaliyo athiriwa na mvua hizo ni pamoja na Malinyi, Mlimba, Masagati na Uchendule ambapo pia ameeleza tuelewe kwamba mvua za mwaka huu zimekuwa kubwa kupita kiasi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...