Na Mwandishi wetu.

SERIKALI mkoani Mara ipo katika hatua za mwisho za kuanza utekelezaji wa mkakati mahsusi wa kukomesha matukio ya uvamizi wa mgodi wa North Mara unaofanywa na baadhi ya vijana wa eneo la Nyamongo na wilaya ya Tarime kwa ujumla.

Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesema kwamba lengo la mkakati huo unaohusisha elimu kwa makundi ya kijamii ni kutengeneza mazingira rafiki yatakayowezesha mgodi wa North Mara kufanya shughuli zake za uchimbaji wa dhahabu bila bughudha huku pia wananchi wakinufaika na uwepo wa mgodi huo.

Wakati serikali mkoani Mara ikiwa katika hatua za mwisho za utekelezaji wa mkakati huo, Kanali Mtambi amewataka vijana kuacha mara moja kuvamia mgodi wa North Mara kwani kufanya hivyo kutazorotesha jitihada hizo zinazolenga kuimarisha amani na kutengeneza mazingira rafiki ya wananchi kunufaika na mgodi huo.

"Mara baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara, miongoni mwa majukumu makubwa niliyokabidhiwa ni kukomesha uvamizi wa mgodi wa North Mara ambao umekuwa ukisababisha vifo na majeraha miongoni mwa vijana" alisema Kanali Mtambi

Aliongeza kwamba yeye kama mkuu wa mkoa hawezi kuruhusu raia kuuawa, lakini pia hatofumbia macho vijana kuvamia mgodi, na ndiyo sababu ameamua kuja na mkakati mahsusi wa kukomesha matukio hayo.

Kwa mujibu wa Kanali Mtambi, siku za karibunii kabla ya kuapishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara, zisikika taarifa za kundi la vijana kuvamia mgodi wa North Mara na kusababisha kifo cha mtu mmoja baada ya kuzuka tafrani baina ya vijana hao na askari polisi wanaolinda mgodi huo.

Kufuatia tukio hilo baadhi ya wanasiasa walilitupia lawama jeshi la polisi wilayani Tarime kwa kuhusika na kifo hicho, lakini Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Tarime na Rorya, Mark Njera alikanusha tuhuma hizo na kusema atatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.

Hata hivyo Kanali Mtambi alisema kwamba chini ya uongozi wake atahakikisha uvamizi unakomeshwa, na vijana kuanza kunufaika na uwepo wa mgodi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...