Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi akipunga mkono kuwaaga mamia ya wananchi, walioongozwa na viongozi wa chama na Serikali Mkoa wa Ruvuma, waliofika Uwanja wa Ndege wa Songea, kumuaga kiongozi huyo baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani humo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 13 iliyomfikisha katika mikoa sita, akianzia Katavi, kisha Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Balozi Nchimbi, ambaye katika ziara hiyo aliambatana na Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni na Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akiwa ziarani kwenye maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo, amekagua na kuhamasisha uhai na ujenzi wa chama.

Aidha, katika ziara hiyo pia, Balozi Nchimbi ametoa maelekezo mbalimbali kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa wizara yaliyolenga kuboresha na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025, hasa maeneo ya miradi ya maendeleo ya wananchi na kuwatumikia watu.

Kupitia ziara hiyo, CCM katika ngazi ya taifa, hasa kupitia kwa Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, imeendeleza utaratibu wake wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea maelekezo kwa ajili ya kuzitatua, huku Gavu akiendelea kuhamasisha wanachama na viongozi kuendelea kukiimarisha CCM na kujiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (2024) na Uchaguzi Mkuu (2025).Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...