KLABU Ya Rotary Dar yaendelea Kuweka Mikakati ya kuchangia ufaulu wa Wanafunzi wa shule za Misingi kwa kuboresha Mazingira rafiki ya Kujisomea kwa kugawa Madawati na kutoa elimu ya Teknohama kwa Walimu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jonas Rwegasira wakati akikabidhi Madawati 1000 kwa Shule tano za Msingi Wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika Leo Aprili 20,2024 Shule ya Msingi Kisauke Jijini Dar es Salaam.

Rwegasira amesema Wadau kama Klabu ya Rotary ni watu ambao wamekuwa wakisaidia sana Serikali katika kuboresha Mazingira rafiki kwa Wanafunzi kujisomea kwa kugawa Madawati kwani Serikali imekuwa ikitafuta Wadau mbalimbali ambao watachochea ufaulu mzuri kwa Wanafunzi hao.

"Wadau hawa Rotary wameenda Kuandika historia nyingine ndani ya mioyo ya watoto hawa pamoja na Shule hizi tano ikiwemo Shule ya Msingi Mtakuja, Kisauke,Salasala,Kunduchi, pamoja na Shule ya Msingi Twiga kwani kila shule imekabidhiwa Madawati 200."

Mratibu wa mradi huo Ezra Kavana amesema Klabu hiyo ina lengo la kuboresha Mazingira mashuleni na mpango huo wa Madawati umeendelea kupewa ushirikiano na Klabu ya Rotary ya Vancouver ambapo Madawati hayo elfu 1000 yamegharimu pesa taslimu Milioni mia moja na ishirini na Saba.

Aidha ameongeza kuwa Klabu hiyo pia inalenga kupanda miti kwa wingi kwani sehemu kubwa ya Madawati hayo ni miti ambayo imekuwa ikikatawa hivyo Kuna umuhimu wa kupanda miti kwa wingi ili Madawati hayo yaendelee kuzalishwa kwa wingi.

"Kila dawati tunalolikabidhi tunahakikisha tunapanda miti miwili ambapo tayari tumeshatekeleza hilo kwa kupanda miti 2500 ."

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kisauke Hamza Suleiman mepongeza Klabu hiyo kwa kuendelea kugawa Madawati kwa Shule za Misingi ili kuleta Ufaulu Mzuri Kwa Wilaya ya Kinondoni.

"Tunakwenda kutengeneza mazingira mazuri ya taaluma kwa watoto wetu madawati haya mia 200 yataenda kuleta chachu ya kuongeza ufaulu wa shule yetu."

Pia ameeleza kuwa bado shule hiyo inapitia changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa,ofisi za walimu pamoja na Matundu ya vyoo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...