Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, jioni ya leo Alhamis Aprili 11, 2024 amehudhuria, akiwa Mgeni Rasmi wa Hafla ya Uzinduzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kiislamu Matemwe, uliofanyika huko ofisini, katika uwanja wa Pangamagae, shehia ya Matemwe Kusini, Wilaya ya Kaskazin 'A' Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Hafla hiyo ambayo imeambatana na viburudisho mbalimbali ikiwemo mashindano ya usomaji Qur-ani, na mchezo wa kuvuta kamba uliowajumuisha waalimu wa madrasa za karibu, pamoja na utoajiwa zawadi, umehudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Dini na Jamii wakiwemo; Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja na Katibu wa Idara ya Habari na Uenezi ACT Wazalendo Taifa, Bw. Othman Ali Maulid na Ndugu Salim Abdallah Biman.
Aidha uongozi wa Chama cha ACT Wazalendo wa Jimbo la Mkwajuni Unguja, wametoa ahadi mbele ya mgeni rasmi ya kutoa vifaa mbali mbali ili kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya jumuiya hio ambayo imetimiza miaka ishirini tangu kuasisiwa kwake.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Aprili 11, 2024.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...