Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo Aprili 23, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali, linalojihusisha na Afya ya Macho Jumuishi na Watu Wenye Ulemavu, ' Christian Blind Mission' (CBM).

CBM lenye Makao yake Makuu Nchini Ujeruman, ambalo limejikita zaidi katika Mpango wa Kuwasaidia Wenye Ulemavu wa Macho, Ujumbe wake umewasili Ofisini kwa Mheshimiwa Makamu wa Kwanza, ili kueleza mafanikio na changamoto mbali mbali walizokutana nazo, katika Harakati zao.

Shirika hilo ambalo lilianza Kazi hapa Visiwani mnamo Mwaka 2022, linatarajia kukamilisha Harakati zake mwishoni mwa Mwaka huu wa 2024.

Viongozi na Waratibu mbali mbali wamehudhuria katika Kikao hicho wakiwemo; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Harusi Said Suleiman; Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Dkt. Omar Dadi Shajak; Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Zanzibar, Dr. Salim Slim; na Mratibu wa Shirika hilo hapa Nchini, Bi. Nesia Mahenge.

Wajumbe wengine waliohudhuria hapo ni kutoka katika Mataifa ya Kenya, Ethiopia, Ujerumani, na wenyeji Tanzania.


Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Aprili 23, 2024.
















 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...