Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akipokea maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa Hospital ya Wilaya wa Magharini "B" Mwanakwerekwe Ijitimai wakati alipofanya ziara ya  kutetembelea na kukagua utowaji wa huduma katika hospitali hio.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya mifupa katika hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja wakati alipofanya ziara ya  kutetembelea na kukagua utowaji wa huduma katika hospitali hio.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ametoa agizo kwa uongozi wa Kampuni ya Lancet kuhakisha ndani ya mwezi mmoja kitengo cha wagonjwa walio katika uangalizi maalum (ICU) katika hospitali ya Wilaya ya Magharibi “B” Mwanakwerekwe Ijitimai kinatoa huduma ili kuondoa usumbufu wa ongezeko la wagonjwa katika hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.

 

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya utowaji na upatikanaji wa huduma za Afya kwa wananchi katika hospital ya Wilaya ya Magharibi “B” Mwanakwerekwe Ijitimai na Hospital ya Taifa ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Mkoa wa Mjini Magharibi.

 

Amesema kuwa Kampuni ya Lancet ina wajibu wa kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatika kwa ubora na haraka kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali zote za Wilaya ili kuondosha msongamano wa wagonjwa katika hospital za Rufaa ya Mnazi Mmoja.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya Awamu ya Nane imelipa kipaombele suala la kuboresha miundombinu ya Afya ili kuzidi kutoa huduma bora za kitabibu kwa Wananchi hivyo wananchi wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi katika kuwaletea maendeleo ikiwemo upatikanaji wa huduma bora za Afya.

 

 Mhe. Hemed amewasisitiza madaktari kudumisha nidhamu katika kazi kwa kufuata miiko, miongozo na maadili ya kazi zao na kuachana na tabia ya kuwatolea lugha chafu wagonjwa hasa wahuduma za Dharura  ili kuendelea kuilinda heshima ya  wananchi ambapo Serikali haitamvumilia mtu yoyote atakae kwenda kinyume na maadili ya kazi na itamchukulia hatua za kisheria na kinidhamu kwa haraka .

 

Aidha Makamu wa Pili wa Rais  amezitaka kampuni ya  Lancet  na NSK zinazotoa huduma katika hospital za Wilaya na Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kuhakikisha changamoto zote za vifaa, wataalamu na kiutendaji zinapatiwa ufumbuzi kwa haraka ili kupunguza malalamiko kwa wananchi ambao wameipa Imani Serikali yao ya kiwatumikia na kuwaletea maendeleo.

 

 

 Sambamba na hayo amewasisitiza wananchi kuendelea  kuzitumia Hospitali za Wilaya katika kutafuta matibabu ambazo zinatoa huduma zote za kitabibu ili kupunguza wingi wa wagonjwa katika hospitali za Rufaa.

 

Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa Serikali kuu itahakikisha inatatua chamgamoto zote zinazoikabili Sekata ya Afya zitapatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuendelea kutoa huduma bora na stahiki kwa wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dkt. MUHIDDIN ABDI MAHMOUD amesema katika kupunguza changamoto ya wataalamu katika Hospitali za Wilaya na Rufaa Wizara ya Afya imeamua kusomesha wafanyakazi wake kwa kuwalazimisha kusomea zile kada ambazo zina upungufu wa madaktari ili kuweza kutoa huduma zilizo bora na kwa wakati.

 

Amesema kuwa Wizara ya Afya imepanga kuandaa utaratibu  wa kuwashauri na kuwashawishi wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu kusomea kozi ambazo zina uhaba wa wataalamu   ikiwemo ICU, Ganzi na Usingizi pamoja na Huduma za dharura ili kuweza kulisaidia Taifa kupata wataalamu wazawa.

 

Kwa upande wao wananchi waliofika hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu wameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea hospitali za Wilaya  na kuwasogezea huduma za matibabu karibu na makazi yao zinazotoa huduma bora na kwa wakati sambamba na kuwashukuru Madaktari kwa huduma bora wanazowapatia wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...