Baada ya Awamu ya kwanza ya Mashindano ya Gofu yaliyofanyika Moshi kumuenzi mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Wanawake ya gofu Lina Nkiya kwa kushindana na sasa ni zamu ya Morogoro wanatarajiwa kuchuana kuanzia April 11, 2024.

Michuano hiyo inayoitwa Lina PG Tour imeandaliwa na familia ya Said Nkya kwa kushirikiana na Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU) kwa lengo la kumuenzi mchezaji huyo aliyekuwa na mchango mkubwa kwenye timu na TLGU.

Lina alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliopeperusha vyema bendera ya Tanzania mwaka 2011 walipotwaa taji la Afrika Mashariki na Kati katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Dar es Salaam.

Makamu Rais wa TLGU Ayne Magombe amesema mashindano hayo yatafanyika katika mikoa tofauti na hiyo yote ni kuendelea kumuenzi mchezaji huyo kwa kuibua vipaji na kushindana.

"Nategemea kuona ushiriki mkubwa wa wachezaji kama ilivyokuwa Moshi tulipata mwitikio mzuri, hiyo yote tunathamini kile ambacho akifanya Lina enzi za uhai wake alikuwa anapenda sana mchezo huu,"amesema..

Mume wa Lina Said Nkiya amesema sababu ya kuzunguka kufanya utalii wa gofu ni kwa kuwa mke wake huyo aliupenda mchezo huo na kuwasaidia wengi hivyo, wanataka kuendeleza pale walipoishia kwa kusaidia wengine kuinuka.

Amesema kama walivyofanya Moshi kwa kutoa zawadi nzuri wataendeleza kwa watakaofanya vizuri katika mikoa yote watakayoenda na kuwahimiza wachezaji mbalimbali kujitokeza na kujisajili ili kushiriki kwa wingi.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...